-
Maandamano makubwa ya wananchi wa Bahrain ya kutaka kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa
Apr 17, 2021 22:02Wananchi wa Bahrain wamefanya maandamano makubwa ambapo sambamba na kulalamikia mazingira mabaya ya wafungwa wa nchi hiyo hasa baada ya kuongeza idadi ya walioambukizwa virusi vya corona miongoni mwao, wametoa wito wa kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa wa nchi hiyo.
-
Tuhuma za matumizi ya silaha za kemikali dhidi ya Syria; mbinu yenye lengo la kudhoofisha mamlaka ya kujitawala Damascus
Apr 17, 2021 21:58Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imepinga ripoti iliyopewa jina la " Timu ya Uchunguzi na Utambuzi" iliyotolewa na Taasisi ya Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW) kuhusu tukio la Saraqib na kuitaja ripoti hiyo kuwa ni ya upotoshaji na ya uongo.
-
Yemen: UN ni mshirika katika uharamia wa Saudia na washirika wake
Apr 17, 2021 03:50Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mafuta la Yemen amekosoa hatua ya muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia wa kuendelea kushikilia meli zinazobeba mafuta kuelekea Yemen na kusema kuwa Umoja wa Mataifa pia ni mshirika katika uharamia huo.
-
Wapalestina 70,000 wamesali Sala ya Ijumaa ya kwanza ya Ramadhani katika ua wa Msikiti wa Al Aqsa
Apr 16, 2021 22:12Licha ya vizuizi vilivyowekwa na askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, maelfu ya Wapalestina wamesali Sala ya Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani katika ua wa msikiti wa Al Aqsa, huko Baitul Muqaddas Mashariki, Palestina inayokaliwa kwa mabavuu.
-
Wapalestina 4,500 wanashikiliwa katika korokoro za utawala ghasibu wa Israel
Apr 16, 2021 07:34Jumuiya ya Mateka wa Kipalestina imetangaza kuwa, Wapalestina 4,500 wakiwemo wanawake 41 na watoto 140 wanaendelea kushikiliwa katika mahabusu za utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Kujaribiwa irada na nguvu ya Iran; kosa la kistratijia la Netanyahu
Apr 16, 2021 03:32Kumetokea mvutano kati ya utawala haramu wa Israel na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufuatia hatua ya utawala huo ya kufanya uharibifu katika kutuo cha urutubishaji urani cha Iran katika eneo la Natanz, uharibifu ambao umetajwa na Iran kuwa ni ugaidi wa kinyuklia.
-
Ndege za kivita za Israel zashambulia Ukanda wa Ghaza
Apr 16, 2021 03:16Ndege za kivita za utawala haramu wa Israel zimetekeleza mashambulizi dhidi ya eneo la Ukanda wa Ghaza mapema leo asubuhi.
-
Mjumbe wa UN: Suluhisho la mgogoro wa Yemen ni la kisiasa
Apr 16, 2021 03:13Martin Griffiths, Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoj wa Mataifa katika masuala ya Yemen amesisitiza kuwa, mgogoro wa Yemen unapaswa kutafutiwa suluhisho la kisiasa.
-
Ansarullah yajibu mapigo baada ya Saudia kuua watoto wa Yemen kwa mabomu
Apr 15, 2021 23:03Wanaharakati wa Ansarullah wakishirikiana na vikosi vya jeshi la Yemen wameshambulia kwa makombora na ndege zisizo na rubani (droni) kituo cha mafuta cha Aramco cha Saudi Arabia, siku moja baada ya muungano vamizi unaoongozwa na Riyadh kushambulia kwa mabomu mkoa wa Sa'ada wa kaskazini magharibi mwa Yemen.
-
Wazayuni wana wasiwasi wa Iran kulipiza kisasi cha hujuma dhidi ya kituo cha nyuklia cha Natanz
Apr 15, 2021 09:08Waziri mkuu wa zamani wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel amesema, ana wasiwasi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuchukua hatua ya kulipiza kisasi kwa sababu ya Israel kufanya hujuma katika kituo cha nyukulia cha Natanz.