-
Ammar al Hakim atilia mkazo ulazima wa askari wa Marekani kuondoka Iraq
Feb 12, 2021 23:25Kiongozi wa Harakati ya Hekima ya Kitaifa ya Iraq amesisitiza kuhusu ulazima wa Marekani kubadilisha mwenendo wake katika Asia Magharibi na askari wa nchi hiyo kuondoka katika eneo hilo.
-
UN: Watoto wasiopungua laki nne wako hatarini kufa kwa njaa mwaka huu nchini Yemen
Feb 12, 2021 23:24Mashirika manne ya utoaji huduma ya Umoja wa Mataifa yametahadharisha kuwa, ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa, watoto wasiopungua laki nne wa umri chini ya miaka mitano wanaweza kupoteza maisha nchini Yemen mwaka huu kutokana na hali mbaya sana ya lisheduni iliyosababishwa na athari za vita na janga la virusi vya corona.
-
Ongezeko la ukandamizaji wa utawala wa Aal Khalifa dhidi ya Wabahrain katika mwaka wa 10 wa mwamko wao
Feb 12, 2021 09:25Wakati ukikaribia mwaka wa 10 tokea uanze mwamko wa wananchi wa Bahrain dhidi ya utawala wa ukoo wa Aal Khalifa nchini humo, utawala huo dhalimu umeshadidisha ukandamizaji na utumiaji mabavu dhidi ya wananchi wanaotaka mabadiliko.
-
Kaulimbiu ya "Kuporomoka Utawala wa Aal Saud" yatamba katika mitandao ya kijamii Saudi Arabia
Feb 12, 2021 07:48Wanaharakati wa mitandao ya kijamii nchini Saudi Arabia wameanzisha kampeni kubwa iliyopewa trend ya "Kuporomoka kwa Utawala wa Aal Saud".
-
Wasiwasi wa UN wa kuendelea kuteswa wanaharakati katika jela za Imarati
Feb 12, 2021 04:10Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Haki za Binadamu ameelezea kusikitishwa na hali mbaya na mateso wanayofanyiwa wanaharakati wa haki za binadamu katika jela za Umoja wa Falme za Kiarabu na ametaka waachiliwe huru.
-
Ansarullah yatoa indhari kwa mashirika ya ndege kutotumia viwanja vya ndege vya Saudia
Feb 11, 2021 04:33Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Asarullah ya Yemen amesisitiza kuwa, Utawala wa Aal Saud unatumia viwanja vya ndege vya Saudia kutekeleza mashambulizi dhidi ya Yemen na kuyatahadharisha mashirika ya ndege kutotumia viwanja hivyo.
-
Ismail Hania atoa mkono wa pongezi kwa maadhimisho ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Feb 11, 2021 04:22Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ametoa mkono wa pongezi na kheri kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na wananchi wa Iran kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 42 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
-
Marekani yaonesha undumakuwili wake kwa kukosoa jibu la Yemen badala ya uchokozi wa Saudia
Feb 11, 2021 00:23Ikulu ya Marekani White House imekosoa jibu la shambulio lililofanywa na ndege zisizo na rubani za Yemen dhidi ya Saudi Arabia badala ya kulaani mashambulio na jinai zinazofanywa na muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na utawala wa Riyadh dhidi ya nchi hiyo.
-
UN: Uamuzi wa ICC umefungua mlango wa kupata haki Wapalestina
Feb 10, 2021 20:05Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya haki za binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amesema uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC wa kubariki kuchunguzwa jinai za utawala wa kigaidi wa Israel dhidi ya taifa la Palestina umefungua mlango wa kupata haki Wapalestina.
-
Abdulsalam: Martin Griffiths ni Muingereza katika joho la Umoja wa Mataifa
Feb 10, 2021 04:18Msemaji wa harakati ya wananchi wa Yemen ya Ansarullah amesema kuwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa Yemen, Martin Griffiths, ni Muingereza aliyevaa joho la Umoja wa Mataifa.