-
Mkuu wa UNRWA atoa indhari: Israel inaelekea kufanya "mauaji ya halaiki ya idadi kubwa" katika Mji wa Ghaza
Oct 03, 2025 07:10Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), Philippe Lazzarini, ametahadharisha kwamba utawala wa kizayuni wa Israel inaonekana unapanga kufanya "mauaji ya halaiki ya idadi kubwa" katika Mji wa Ghaza huku ukiwa unashadidisha mzingiro wake na mashambulizi makubwa ya kijeshi dhidi ya mji huo.
-
Pakistan: Mpango wa Trump kuhusu Ghaza ni tofauti na ulioidhinishwa na viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu
Oct 03, 2025 07:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Ishaq Dar amesema mpango wa amani wa vipengele 20 uliopendekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump kwa ajili ya Ghaza sio ule ulioidhinishwa na viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu, ikiwemo Pakistan.
-
Mauaji ya Kimbari ya Marekani na Israel Gaza: Idadi ya vifo yapanda hadi 66,225
Oct 03, 2025 04:19Vikosi katili vya Israel vinaendelea kuongeza ukatili dhidi ya raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, vikisababisha vifo na majeraha kwa idadi kubwa ya watu, hususan katika maeneo ya kati na kusini mwa eneo hilo.
-
Kiongozi wa Ansarullah Yemen: Mpango wa Trump kuhusu Gaza ni 'ramani ya Kizayuni' ya kufuta haki za Wapalestina
Oct 03, 2025 04:14Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah nchini Yemen amesema kuwa mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Ukanda wa Gaza baada ya vita ni “ramani ya Kizayuni” inayolenga kufuta haki za Wapalestina na kuimarisha udhibiti wa eneo hilo.
-
Watumiaji X katika kuunga mkono msafara wa Sumud: Kila meli ni sauti ya kutaka uhuru wa Palestina
Oct 03, 2025 03:32Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa "X" wameuita msafara wa kimataifa wa meli nyingi wa Sumud kuwa meli ya ukarimu na utu wa binadamu.
-
Hamas: Mashambulizi ya Israel dhidi ya msafara wa Sumud ni 'ugaidi wa baharini'
Oct 03, 2025 00:01Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imelaani vikali mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya msafara wa kimataifa wa meli nyingi wa Sumud ukielekea Ukanda wa Gaza.
-
Afrika Kusini yaitaka Israel iwaachie wanaharakati wa msafara wa Sumud
Oct 03, 2025 00:00Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa jana Alkhamisi alitaka kuachiliwa mara moja kwa Waafrika Kusini na raia wengine wa kigeni wanaozuiliwa na jeshi la Israel, baada ya wanajeshi wa majini wa utawala huo haramu kushambulia msafara wa kibinadamu uliokuwa unaelekea Gaza.
-
Maandamano makubwa Ulaya kupinga hujuma ya Israel dhidi ya msafara wa Sumud
Oct 02, 2025 08:40Maandamano makubwa yameshuhudiwa katika nchi za Ulaya kupinga mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya uvamizi wa meli ya msafara wa kimataifa wa Sumud.
-
Gazeti la New York Times lafichua jinai za kivita za Marekani nchini Afghanistan
Oct 02, 2025 08:33Ripoti ya uchunguzi ya New York Times imefichua undumakuwili na kinga ya wanajeshi wa Marekani wanaotuhumiwa kwa uhalifu wa kivita nchini Afghanistan, ikihusisha kesi kama vile mauaji ya raia, utesaji na shambulio la hospitali ya Madaktari Wasio na Mipaka na kutofunguliwa mashtaka na kupewa adhabu kali kwa wahusika.
-
Jinai za Marekani wakati wa uvamizi wa Iraq
Oct 02, 2025 04:56Jinai za Marekani wakati wa kuikalia kwa mabavu Iraq zilikuwa kubwa na mfano mchungu sana wa mauaji na uharibifu chini humo ambazo wavamizi wa Kimarekani walijaribu na hadi sasa wanaendelea kujaribu kuzihalalisha kwa majina tofauti ya udanganyifu.