-
Jihadul Islami, Ansarullah zapinga mpango wa Trump-Netanyahu kuhusu Gaza
Oct 01, 2025 07:21Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Jihadul Islami ya Palestina amekosoa vikali mpango wa Rais Donald Trump wa Marekani wenye vipengele 20 wa eti kumaliza vita vya mauaji ya halaiki ya Israel dhidi ya Gaza, na kuutaja kama "mfumo wa kuendeleza uchokozi na uvamizi wa Israel dhidi ya taifa la Palestina."
-
Mpango wa Trump wa vipengele 20, tapatapa ya kuuokoa utawala wa kizayuni usishindwe katika vita vya Ghaza
Oct 01, 2025 05:58Makundi ya Muqawama katika eneo hili la Asia Magharibi yakiwemo ya Jihadul-Islami ya Palestina na Ansarullah ya Yemen yameuelezea mpango wa Rais Donald Trump wa Marekani kwa ajili ya Ghaza kuwa ni jaribio la kutapatapa la kuuokoa utawala wa kizayuni wa Israel usishindwe katika vita vya mauaji ya kimbari ulivyoanzisha dhidi ya eneo hilo la Palestina uliloliwekea mzingiro.
-
Makombora ya Yemen yafunga uwanja wa ndege wa pili wa Israel
Oct 01, 2025 03:01Miaka sita baada ya kufunguliwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ramon kwa kelele na mbwembwe nyingi, ukiwa ni uwanja wa ndege wa pili kwa ukubwa wa utawala wa Kizayuni, sasa hivi mashambulizi ya wanamapambano ya Yemen yamepelekea kufungwa kabisa uwanja huo kama sehemu ya Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa iliyoongozwa na HAMAS miaka miwili iliyopita.
-
Mashirika ya silaha ya Israel yakumbwa na janga la kusambaratika
Oct 01, 2025 03:00Kadiri jinai na mauaji ya kimbari ya Israel yanavyozidi kuongezeka huko Ghaza, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Lebanon ndivyo ususiaji wa kimataifa unavyozidi kushika kasi na sasa hivi mashirika ya silaha ya utawala wa Kizayuni yanakabiliwa na janga la kusambaratika kutokana na uvundo wake kuhinikiza kila sehemu duniani.
-
Yemen: Tuko tayari kuungana na 'jeshi la kimataifa' linalopendekezwa na Colombia kuikomboa Palestina
Sep 30, 2025 23:04Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amepongeza pendekezo la hivi karibuni la Rais wa Colombia wakati wa hotuba yake mbele ya Umoja wa Mataifa la kuundwa 'jeshi la kimataifa' litakalopewa jukumu la kuikomboa Palestina kutokana na uvamizi na uporaji wa ardhi unaoungwa mkono na Marekani.
-
Russia: Hatutashiriki kwenye mpango wa Trump kuhusu Gaza
Sep 30, 2025 23:03Sambamba na kusisitizia utayarifu wa Russia wa kutatua mgogoro wa Asia Magharibi, Msemaji wa Ikulu ya Russia (Kremlin) amesisitiza kuwa Moscow haitashiriki katika mpango wa Rais wa Marekani juu ya Ukanda wa Gaza.
-
Katibu Mkuu wa Jihadul-Islami ya Palestina, Ansarullah ya Yemen 'wauponda' mpango wa Trump kuhusu Ghaza
Sep 30, 2025 03:35Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesisitiza kwamba, mpango wa Donald Trump kwa ajili ya Ukanda wa Ghaza ni mpango wa utawala wa Kizayuni na ni waraka wa agizo la kuendeleza uchokozi na uvamizi dhidi ya wananchi wa Palestina.
-
Hamas: Mpango wa Trump 'hauna mpango', hauna dhamana
Sep 29, 2025 23:26Rais wa Marekani ambaye ndiye chanzo kikuu cha mauaji ya umati huko Ghaza kwa uungaji mkono wake wa hali ya juu kwa utawala wa Kizayuni, kwa mara nyingine tena amejifanya eti anataka kukomeshwa vita Ghaza, sambamba na kuiunga mkono kikamilifu Israel. HAMAS imepinga mpango huo ikisisitiza kuwa hauna jipya na hauna dhamana yoyote ya kutekelezwa.
-
Israel yasitisha huduma uwanja wa ndege wa Tel Aviv kufuatia mashambulizi ya Yemen
Sep 29, 2025 23:00Uwanja wa ndege mkuu wa Israel umesimamisha kwa muda safari za ndege baada ya jeshi la Yemen kufanya operesheni maalumu ya shambulizi kwa kutumia kombora la 'hypersonic' aina ya Palestina 2 na ndege zisizo na rubani dhidi ya miji ya Tel Aviv na Eilat ya utawala wa kizayuni wa Israel.
-
HAMAS: Tony Blair 'ndugu wa shetani' ni wa kupandishwa kizimbani, si wa kuiongoza Ghaza
Sep 29, 2025 07:16Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani mpango ulioripotiwa kuwa umeandaliwa na Marekani wa kumteua waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair awe liwali wa Ukanda wa Ghaza, na kusisitiza kwamba watu wa Palestina wanao uwezo wa kusimamia mambo yao wenyewe.