-
Jibu la hapana la Indonesia kwa takwa la kuanzisha uhusiano wa kawaida na Wazayuni
Jan 04, 2021 23:18Serikali ya Indonesia imetoa jibu la hapana kwa juhudi zinazoitaka ianzishe uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
-
Ripoti: Saudia imetekeleza mashambulio 8,888 ya anga dhidi ya Yemen 2020
Jan 04, 2021 12:06Msemaji wa Majeshi ya Yemen ametoa takwimu za mashambulio ya muungano vamizi wa Saudi Arabia dhidi ya wananchi wa Yemen, na mafanikio ya vikosi vya Yemen dhidi ya wavamizi hao katika mwaka uliomalizika wa 2020.
-
Nasrallah: Iran inaweza kulipiza kisasi mauaji ya Shahidi Soleimani wakati wowote itakapo
Jan 04, 2021 00:04Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni nchi yenye nguvu na uwezo na kuongeza kuwa, wakati wowote itakapo, na bila kuhitajia waitifaki wake wa eneo, Iran inaweza kulipiza kisasi mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani.
-
Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi: Tutaendelea kuienzi damu toharifu ya makamanda wa ushindi
Jan 03, 2021 10:08Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi ya Iraq amesema, hatua ya mwanzo kabisa ya kulipiza kisasi cha mashahidi Qassem Suleimani na Abu Mahdi al-Muhandis ni kula kiapo tena cha utiifu kwao na kuendeleza njia yao.
-
Watalii kutoka Israel waingiza kimagendo madawa ya kulevya nchini Imarati
Jan 03, 2021 09:59Baadhi ya vyombo vya habari vya Kiebrania vimetangaza kuwa, watalii kutoka Israel wanaoelekea Umoja wa Falme za Kiarabu wanaingiza kimagendo madawa ya kulevya katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Waziri wa Ulinzi wa Yemen atahadharisha juu ya uwepo wa wanajeshi wa Kizayuni katika maeneo yaliyovamiwa
Jan 03, 2021 03:21Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen amesema kuwa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wapo katika vituo vya kijasusi katika maeneo yaliyokaliwa kwa mabavu na muungano vamizi huko Yemen unaaongozwa na Saudi Arabia.
-
Wairaq kufanya maandamano mamilioni leo kukumbuka siku waliyouawa shahidi makamanda wa muqawama
Jan 02, 2021 23:24Mbunge wa mrengo wa As-Sadiqun katika bunge la Iraq amesema, lengo la maandamano makubwa yatakayofanywa leo na wananchi wa Iraq kwa mnasaba wa kukumbuka siku walipouliwa shahidi makamanda wa muqawama ni kutangazwa upinzani dhidi ya uwepo kijeshi wa Marekani katika ardhi ya nchi hiyo.
-
Mateka 15 Wapalestina walioko kwenye gereza la Israel la An-Naqb wameambukizwa corona
Jan 02, 2021 23:23Ofisi ya habari inayoshughulikia masuala ya mateka Wapalestina imetangaza kuwa mateka 15 Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye jela ya Kizayuni ya An-Naqb wameambukizwa virusi vya corona.
-
Mamluki wa Saudia wahujumu harusi nchini Yemen, waua watu watano
Jan 02, 2021 09:31Mamluki wanaoungwa mkono na Saudi Arabia wamevamia sherehe ya harusi katika mji wa bandarini wa Al Hudaydah nchini Yemen na kuua watu wasiopungua watano na kuwajeruhi wengine kadhaa wakiwemo wanawake saba.
-
Majina ya watuhumiwa wa mauaji ya shahid Soleimani kutangazwa karibu hivi
Jan 02, 2021 03:56Kiongozi mmoja wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la al Hashd al Shaabi amesema kuwa, siku chache zijazo idara ya mahakama ya Iraq itatangaza majina ya watuhumiwa wa mauaji ya makamanda wa muqawama akiwemo shahid Luteni Jenerali Qassem Soleimani.