Majina ya watuhumiwa wa mauaji ya shahid Soleimani kutangazwa karibu hivi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i65537-majina_ya_watuhumiwa_wa_mauaji_ya_shahid_soleimani_kutangazwa_karibu_hivi
Kiongozi mmoja wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la al Hashd al Shaabi amesema kuwa, siku chache zijazo idara ya mahakama ya Iraq itatangaza majina ya watuhumiwa wa mauaji ya makamanda wa muqawama akiwemo shahid Luteni Jenerali Qassem Soleimani.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Jan 02, 2021 03:56 UTC
  • Majina ya watuhumiwa wa mauaji ya shahid Soleimani kutangazwa karibu hivi

Kiongozi mmoja wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la al Hashd al Shaabi amesema kuwa, siku chache zijazo idara ya mahakama ya Iraq itatangaza majina ya watuhumiwa wa mauaji ya makamanda wa muqawama akiwemo shahid Luteni Jenerali Qassem Soleimani.

Mtandao wa habari Saberin News umemnukuu Mohannad al Aqabi, mkurugenzi wa vyombo vya habari wa harakati ya al Hashd al Shaabi akisema hayo usiku wa kuamkia leo Jumamosi na kuongeza kuwa, kuna watuhumiwa 40 katika kesi ya mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH baadhi yao ni Wairaq na wengine ni Wamarekani.

Al Aqabi amesisitiza kuwa, licha ya kwamba mahakama ya Iraq iko chini ya mashinikizo ya ndani na nje, lakini imefanya kazi kubwa ya kuwatambua watuhumiwa na siku chache zijazo majina ya watuhumiwa hayo yatatangazwa hadharani.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Mkuu wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Mkuu wa Harakati ya al Hashd al Shaabi na wanamapambano wenzao wanane, waliuliwa kigaidi na kidhulma na wanajeshi magaidi wa Marekani, tarehe 3 Januari 2020 katika shambulio la anga lililofanywa na magaidi hao karibu na uwanja wa ndege wa Iraq, akiwa mgeni rasmi wa serikali ya nchi hiyo.