IRGC: Vikizuka vita vipya, Iran itatumia silaha zinazosababisha uharibifu mkubwa zaidi
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa, kama vitazuka vita vipya litatumia silaha zinazosababisha uharibifu mkubwa zaidi na za kisasa zaidi kuliko zile zilizotumika katika vita vilivyopita.
Msemaji wa IRGC Brigedia Jenerali Hossein Mohebbi ametoa kauli hiyo leo Alkhamisi wakati akifafanua kuhusu uwezo wa kijeshi wa Iran na maendeleo ya vichwa vya makombora baada ya vita vya siku 12 na siku 40 vilivyoanzishwa na Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu mnamo Juni 2025 na mwishoni mwa Februari mwaka huu.
Mohebbi amesema, nguvu ya uharibifu na uteketezaji ya vichwa vya makombora vilivyotumika katika makombora ya IRGC mara hii ni kubwa zaidi kuliko ile iliyotumika katika vita vya huko nyuma.
Ameongeza kuwa Iran inapiga hatua za ustawi kiuendelevu katika maeneo yote ya silaha za kijeshi, kwa kuunda silaha ambazo zinalenga shabaha kwa usahihi zaidi, zenye nguvu ya kuteketeza zaidi na za kisasa zaidi kiteknolojia.
"Ikiwa vita vingine vitaanza, bila shaka silaha zetu zitakuwa tofauti na zilizopita. Tofauti hii inaweza kuonekana katika uzalishaji wa vichwa vya makombora, mifumo ya usahihi wa kushambulia, masafa ya makombora, au eneo lingine lolote," ameeleza Jenerali Mohebbi.
Msemaji wa IRGC amesisitiza kwamba Iran haijawahi kusimamisha uzalishaji na uundaji wa silaha, na akaongezea kwa kusema: "Tunapiga hatua kimaendeleo kila siku, na kuna muelekeo wa kujitokeza sinario yoyote katika uwanja huu."
Mnamo mwezi uliopita wa Julai, Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Majid Ibn Reza alisema, mitambo ya uzalishaji inafanya kazi kwa kasi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo kabla, akisisitizia azma ya Jamhuri ya Kiislamu ya kuwa na muundo maalumu wa mustakabali wake wa kiulinzi…/