-
Msemaji wa Jeshi la SEPAH: Marekani haina uwezo tena wa kuendelea kuwepo Asia Magharibi
Sep 10, 2026 03:22Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema kuwa Marekani haina uwezo tena wa kuendelea kuwepo katika eneo la Asia Magharibi.
-
Meja Jenerali Vahidi: Damu isiyo na hatia ya mashahidi madhulumu wa Kohestak haitapotea
Sep 04, 2026 03:20Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe maalumu na kusema kuwa: Damu isiyo na hatia ya mashahidi waliouliwa kidhulma na magaidi wa Kimarekani huko Kohestak haitapotea kamwe na wahusika wakiwemo makamanda waliofanya jinai hiyo ya kivita wataburuzwa mahakamani.
-
Baada ya shambulio harusini; IRGC yasema: Viongozi wa US wanapasa kuwajibishwa kwa jinai za kivita
Sep 03, 2026 10:17Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limetangaza kuwa Washington lazima iwajibishwe kwa jinai za kivita zilizofanywa na wanajeshi magaidi wa Marekani katika Mkoa wa Hormozgan kufuatia shambulio la anga lililolenga sherehe ya harusi.
-
IRGC yapiga makao ya kamandi ya Marekani na eneo la kuegeshea droni huko Kuwait
Sep 02, 2026 12:57Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limesema kuwa vikosi vyake vimeshambulia makao makuu ya kamandi na makazi ya wanajeshi wa Marekani katika Kituo cha Jeshi la Anga cha Ali Al-Salem nchini Kuwait, na kuteketeza ghala la ndege zisizo na rubani (droni) na eneo la maandalizi ya kurushia ndege hizo. Shambulizi hilo limeharibu idadi kadhaa ya ndege zisizo na rubani za jeshi la kigaidi la Marekani.
-
IRGC: Vikizuka vita vipya, Iran itatumia silaha zinazosababisha uharibifu mkubwa zaidi
Aug 20, 2026 11:51Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa, kama vitazuka vita vipya litatumia silaha zinazosababisha uharibifu mkubwa zaidi na za kisasa zaidi kuliko zile zilizotumika katika vita vilivyopita.
-
Kamanda wa IRGC aonya: Adui ajiandae na "mshtukizo wa kimkakati" wa mashambulizi ya Iran
Aug 17, 2026 06:10Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameonya kwamba, japokuwa hatua za kijeshi za Iran hadi sasa zimebaki kuwa za kujihami tu tangu ulipoanzishwa uadui wa kijeshi dhidi ya taifa hili, lakini vikosi vya jeshi vimejiandaa kikamilifu kuchukua hatua ya kushambulia endapo italazimu, huku akiwaonya maadui kutarajia "mshtukizo wa kimkakati."
-
Iran yaonyesha mabaki ya ndege za kivita za Marekani na Israel ilizozitungua +Video
Aug 15, 2026 03:54Iran imeonyesha sehemu za vifaa vilivyopatikana kutoka ndege za kivita zisizo na rubani (droni) za Marekani na Israel, pamoja na ndege ya kivita ya F-15 ambazo zilitunguliwa kwa mifumo ya ulinzi ya Iran wakati wa vita. Mifumo ya ulinzi iliyotumika kutungua ndege hizo za adui imeundwa hapa nchini.
-
IRGC: Watu 8 wenye silaha wenye mfungamano na makundi ya kigaidi watiwa nguvuni kusini-mashariki mwa Iran
Aug 06, 2026 11:06Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimetangaza kuwa kimewatia nguvuni watu wanane wenye silaha wenye mfungamano na makundi ya kigaidi katika mkoa wa Sistan na Baluchestan kusini-mashariki mwa Iran kufuatia oparesheni maalum mtawalia.
-
IRGC yazionya Israel na Uingereza kuhusu kuisaidia Marekani katika vita dhidi ya Iran
Jul 26, 2026 13:20Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limezionya Uingereza na utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kuisaidia na kushirikiana na Marekani katika vita vyake vya jinai na uchokozi dhidi ya Iran.
-
IRGC yashambulia kambi za Marekani Kuwait na Bahrain, yaonya raia wakae mbali na maeneo walipo Wamarekani
Jul 25, 2026 03:11Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa kutekeleza mashambulizi mapya dhidi ya ngome za kijeshi za Marekani nchini Kuwait na Bahrain, huku likitoa onyo kwa raia katika nchi zinazowapa hifadhi wanajeshi wa Marekani kuondoka mara moja na kuwa mbali kwa angalau mita 500 kutoka maeneo yanayotumiwa na wanajeshi hao.