-
Hamas yatoa wito wa msimamo wa pamoja wa Kiislamu dhidi ya Israel katika Mkutano wa Doha
Sep 15, 2025 01:06Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina,, Hamas, imelaani vikali shambulio la hivi karibuni la Israel dhidi ya Qatar, ikilitaja kuwa ni tendo la “ waoga,” na kutoa wito kwa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kuchukua msimamo wa pamoja dhidi ya hujuma za utawala huo wa kibeberu.
-
Familia za mateka: Netanyahu ndiye kikwazo cha kuwarudisha mateka nyumbani
Sep 15, 2025 00:30Familia za mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS kwa mara nyingine tena zimemtuhumu Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel kuwa kikwazo cha kufikiwa makubaliano ya kuachiliwa ndugu zao.
-
Viongozi wa nchi za Kiislamu na Kiarabu wakutana Doha baada ya shambulio la Israel dhidi ya Qatar
Sep 14, 2025 07:38Viongozi wa mataifa ya Kiislamu na Kiarabu wanakutana katika mji mkuu wa Qatar, Doha kujadili jibu rasmi na la pamoja la kutoa kwa shambulizi la kigaidi lililofanywa na Israel dhidi ya Doha wiki iliyopita, ambalo utawala huo wa kizayuni ulisema liliulenga uongozi wa harakati ya Hamas. Shamnbulio hilo limelaaniwa vikali katika eneo na kila pembe ya dunia.
-
Madaktari 17 wa kigeni waliohudumu Ghaza: Tumepokea watoto 114 waliopigwa risasi kichwani na kifuani
Sep 14, 2025 07:32Madaktari wa kimataifa wanaohudumu katika Ukanda wa Ghaza wameripoti hali ya kushtusha na kuhuzunisha ya majeraha ya risasi walizopigwa watoto Wapalestina, na kuibua wasiwasi wa kwamba watoto hao wamelengwa kwa makusudi. Hayo ni kwa mujibu wa uchunguzi uliochapishwa na gazeti la kila siku la Uholanzi la de Volkskrant.
-
Nafasi ya OIC katika kukabiliana na uchokozi wa utawala wa Kizayuni; mtihani kwa mshikamano wa Ulimwengu wa Kiislamu
Sep 14, 2025 07:24Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameenda Doha leo Jumapili kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC.
-
Waziri wa Israel: Upo uwezekano wa kuwaua viongozi wa HAMAS walioko Uturuki
Sep 14, 2025 07:18Waziri wa Nishati wa utawala wa kizayuni wa Israel, Eli Cohen ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Usalama na Kisiasa, amesema, upo uwezekano wa kuwaua kigaidi viongozi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS walioko Istanbul, Uturuki, na amedai pia katika mahojiano aliyofanyiwa jana Jumamosi na tovuti ya Saudi Elaf kwamba "mtu yeyote anayehusishwa na Hamas hawezi kulala kwa amani popote duniani."
-
Israel yaua waandishi habari 24 wa Yemen ikijaribu kunyamazisha sauti ya haki
Sep 14, 2025 03:33Katika kile kinachoonekana kama kuongezeka kwa kampeni ya kigaidi ya wazi na ya kunyamazisha sauti ya haki, utawala haramu wa Israel umetekeleza mojawapo ya mashambulio mabaya zaidi dhidi ya waandishi wa habari katika historia ya kisasa, kwa kuwalenga na kuwaua angalau waandishi 25 wa habari wa Yemen mjini Sana’a.
-
Ndege za kivita za Israel zilituma makombora ya anga za mbali juu ya Saudi Arabia kushambulia Doha
Sep 14, 2025 03:21Utawala wa Israel ulitumia ndege za kivita kurusha makombora katika anga za mbali juu ya anga ya Saudi Arabia katika shambulio lake la hivi karibuni dhidi ya viongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Mapambano ya Ukombozi wa Palestina, Hamas, waliokuwa mjini Doha, mji mkuu wa Qatar.
-
Ripoti: Mossad yaahirisha mpango wa hujuma ya nchi kavu dhidi ya Hamas Nchini Qatar
Sep 13, 2025 23:55IQNA – Shirika la ujasusi la Israel, Mossad, limeahirisha mpango wa uvamizi wa nchi kavu uliolenga kuwaua viongozi wa Hamas walioko Qatar, mpango uliokuwa ukifanyiwa kazi katika wiki za hivi karibuni.
-
Jeshi la Israel laua Wapalestina wanne waliokuwa wakitafuta msaada Gaza, njaa yashadidi
Sep 13, 2025 23:13Jeshi la Israel limefyatua risasi dhidi ya kundi la Wapalestina waliokuwa wakitafuta msaada wa kibinadamu huko Gaza, na kuwaua angalau watu wanne, huku hospitali katika eneo hilo lilozingirwa zikiripoti vifo zaidi vinavyotokana na njaa na utapiamlo.