-
Jeshi la Yemen lashambulia maeneo nyeti ya Israel kwa kombora la kasi ya juu la “Palestine-2”
Sep 13, 2025 08:11Jeshi la Yemen limetangaza kuwa limevurumisha kombora la kasi ya juu au haipasoniki aina ya “Palestine-2” lenye vichwa vingi vya mlipuko dhidi ya maeneo nyeti ndani ya Tel Aviv, katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu yaani 'Israel'.
-
Je, dunia mara hii ina nia ya kufanikisha kuasisiwa nchi huru ya Palestina?
Sep 13, 2025 07:52Katika hatua ya kihistoria, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio lililopendekezwa na Ufaransa na Saudi Arabia, na kutangaza kuunga mkono kuanzishwa kwa nchi huru la Palestina na kutekelezwa njia ya ufumbuzi wa serikali mbili.
-
UNICEF: Mtoto mmoja kati ya watano wa Kipalestina ana utapiamlo
Sep 13, 2025 03:40Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, hali ya watoto wa Kipalestina hususan katika Ukanda wa Gaza ni mbaya mno na kwamba, mtoto mmoja kati ya watano wa Kipalestina ana utapiamlo.
-
Lavrov: Lengo la Israel ni kudhoofisha uwezekano wa kuundwa taifa huru la Palestina
Sep 13, 2025 03:39Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesisitiza kwamba, hatua za utawala wa Kizayuni zinaonyesha njama zake za kudhoofisha mkakati wa kuundwa "Nchi ya Palestina".
-
Netanyahu aapa hakutakuwa na Dola la Palestina, asisitiza ardhi yote ni milki ya wazayuni
Sep 12, 2025 06:58Waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kuwa, hakutakuwa na dola la Palestina, na kusisitiza kwamba ardhi zote za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo haramu ni milki ya wazayuni.
-
Hamas: Hakuna shaka Marekani imehusika na shambulio la Doha
Sep 12, 2025 03:27Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imelaani vikali ushirikiano wa Marekani na Israel katika shambulizi la anga dhidi ya Qatar na jaribio la mauaji dhidi ya viongozi wa kundi hilo hilo la kupigania ukombozi wa Palestina, ikisisitiza kuwa Washington na Tel Aviv zinataka kusambaratisha mazungumzo ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.
-
Kikao cha dharura cha mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kufanyika Qatar kujadili mashambulio ya Israel
Sep 11, 2025 23:51Mji mkuu wa Qatar Doha utakuwa mwenyeji wa mkutano wa dharura wa kilele wa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu Jumapili na Jumatatu ijayo kuchunguza mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu yaliyolenga makao ya viongozi wa HAMAS.
-
Waziri Mkuu wa Qatar: Benjamin Netanyahu anapasa 'kufikishwa mbele ya sheria'
Sep 11, 2025 07:34Waziri Mkuu wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al-Thani amelaani mashambulizi ya juzi ya Israel dhidi ya Doha na kuyataja kuwa ni "ugaidi wa kiserikali,". Amesema kuwa Waziri Mkuu wa utawala wa Israel Benjamin Netanyahu anapasa "kufikishwa mbele ya sheria."
-
UNRWA: Zaidi ya wakimbizi laki moja wa Gaza hawajapokea msaada wowote tangu miezi 6 iliyopita
Sep 11, 2025 07:34Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetangaza kuwa, zaidi ya watu laki moja wanaendelea kutaabika na njaa katika maeneo ya kuwahifadhi wakimbizi ya shirika hilo huko Gaza, na hakuna msaada wa kibinadamu ambao umeruhusiwa kuingia katika eneo hilo kwa zaidi ya miezi 6 sasa.
-
Baada ya kuzuia mashambulizi mengi ya Israel; Yemen yatoa onyo kali kwa Tel Aviv, yasema Wazayuni wajiandae
Sep 11, 2025 03:51Yemen imetoa onyo kali kwa utawala wa Kizayuni kuhusu uwezekano wa Sana’a kulipiza kisasi vikali dhidi ya mashambulizi ya kinyama ya Tel Aviv huko Yemen.