UNICEF: Mtoto mmoja kati ya watano wa Kipalestina ana utapiamlo
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, hali ya watoto wa Kipalestina hususan katika Ukanda wa Gaza ni mbaya mno na kwamba, mtoto mmoja kati ya watano wa Kipalestina ana utapiamlo.
Ripoti ya UNICEF inaeleza kuwa, hali ya watoto katika Ukanda wa Gaza inazidi kuwa mbaya, na wanakabiliwa na hatari zaidi kutokana na vita, uvamizi wa Israel, na mzingiro mkali dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetahadharisha kuhusu kuzidi kuwa mbaya hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza kutokana na kuendelea mzingiro wa kikatili wa eneo hilo na mzingiro wa Wazayuni wa chakula na dawa, sambamba na kushadidi hujuma za kijeshi dhidi ya eneo hilo.
UNICEF inaeleza kuwa hali ya watoto katika Ukanda wa Gaza inazidi kuwa mbaya, na wanakabiliwa na hatari zaidi kutokana na vita, uvamizi wa Israel, na mzingiro mkali dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Shirika hilo limeripoti ongezeko kubwa la utapiamlo miongoni mwa watoto huko Gaza, huku kiwango kikifikia 13.5% mwezi uliopita.
Wakati huo huo, kufuatia kuenea kwa janga la njaa katika Ukanda wa Gaza, maonyo ya kimataifa kuhusu mzozo wa kibinadamu katika ukanda huo yanaendelea kuongezeka, na Tess Ingram, msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), ameonya juu ya hali inayoongezeka ya njaa katika mji wa Gaza, na kusema kwamba ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa, hatari hii itaenea katikati mwa Ukanda wa Gaza ndani ya wiki chache.