-
Je, inatosha kwa nchi za Magharibi kulaani kwa maneno matupu jinai za utawala wa Israel?
Aug 25, 2025 23:12Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi 21 za Magharibi kwa pamoja wamelaani uamuzi wa Israel wa kujenga makaazi mapya ya walowezi wa Kizayuni huko Quds Mashariki.
-
Hamas, Jihadul Islami zalaani uvamizi wa kifashisti wa Israel dhidi ya Yemen
Aug 25, 2025 07:14Harakati za Muqawama wa Kiislamu za Palestina za Hamas na Jihadul Islami zimeshutumu vikali mashambulizi mabaya ya Israel dhidi ya mji mkuu wa Yemen na miundombinu ya kiraia, na kuyaelezea kama "ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa" na gharama ya kuilinda Palestina.
-
Israel yaendelea kumwaga damu za wanahabari Gaza, yaua wengine 4
Aug 25, 2025 07:06Kwa akali wanahabari wanne wa Kipalestina, akiwemo mpiga picha wa televisheni ya Al-Jazeera, ni miongoni mwa watu 15 waliouawa shahidi katika shambulio jipya la Israel dhidi ya hospitali moja iliyoko kusini mwa Ukanda wa Gaza.
-
Tangu Agosti 6, jeshi la Israel limebomoa kikamilifu majengo zaidi ya 1,000 ya Mji wa Ghaza
Aug 25, 2025 03:29Shirika la Ulinzi wa Raia la Palestina limetangaza kuwa jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limebomoa kikamilifu majengo zaidi ya 1,000 katika vitongoji vya Zeitoun na Sabra katika Mji wa Ghaza tangu lilipoanza kuuvamia mji huo mnamo Agosti 6, na hivyo kupelekea mamia ya Wapalestina kunasa chini ya vifusi vya majengo hayo.
-
Mawaziri wa kizayuni watoa msimamo kuhusu Ghaza: "Wazingireni, waacheni wafe kwa njaa"
Aug 25, 2025 03:08Mawaziri wa utawala wa kizayuni wa Israel wenye misimamo mikali ya chuki wametetea waziwazi hatua ya kuwatesa kwa njaa Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.
-
OIC leo inajadili mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza na kuunganisha pamoja misimamo
Aug 24, 2025 23:29Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) wanafanya mkutano wa dharura leo Jumatatu katika mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia kujadili vita vya mauaji ya kimbari vya Israel huko Gaza na kuunganisha misimamo yao kuhusu mauaji yanayofanywa na Israel katika ukanda huo.
-
Hamas yapongeza 'ujasiri' wa mawaziri wa Uholanzi kujiuzulu juu ya Gaza
Aug 24, 2025 23:27Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imepongeza hatua ya kujiuzulu mawaziri kadhaa wa Uholanzi, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Caspar Veldkamp, kujibu hatua ya kukataa kwa serikali yao kuiwekea vikwazo Israel. Hamas imetaja kujiuzulu huko kama uamuzi wa kijasiri na wa kimaadili.
-
Jaribio la Wazayuni la kumuua kigaidi Mkuu wa Majeshi ya Yemen lagonga mwamba
Aug 24, 2025 23:00Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti habari ya kufeli jaribio la utawala haramu wa Israel la kumuua Mkuu wa Majeshi ya Yemen, kwa mara ya pili sasa.
-
WHO: Zaidi ya watu 15,600 wakiwemo watoto 3,800 wanahitaji kuondolewa haraka Gaza kwa ajili ya matibabu
Aug 24, 2025 08:23Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameeleza kuwa watu zaidi ya 15,600 katika Ukanda wa Gaza, wakiwemo watoto 3,800, wanahitaji kuondolewa haraka katika eneo hilo lililokumbwa na vita ili kupata huduma maalumu ya matibabu.
-
Mkuu wa UNRWA: Nchi zenye ushawishi zichukue hatua dhidi ya Israel kuhusu baa la njaa Gaza
Aug 24, 2025 04:27Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Palestina (UNRWA) Jumamosi ameutaka utawala wa Israel uwajibike kuhusu kusababisha baa la njaa katika Ukanda wa Gaza huku akitoa wito kwa mataifa yenye ushawishi kuchukua hatua mara moja kumaliza mzozo huo.