-
Makumi ya watu wafariki dunia katika ajali ya ndege ya abiria, Russia
Jul 24, 2025 07:01Ndege ya abiria ya Russia imeanguka mapema leo Alhamisi katika eneo la Amur Mashariki mwa nchi, ikiwa na abiria 49. Taasisi ya Huduma za Dharura za Russia inaamini kuwa watu wote 49 waliokuwa katika ndege hiiyo wamefariki dunia.
-
Brazil yajiunga katika kesi ya ICJ dhidi ya mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel Ghaza
Jul 24, 2025 03:18Wizara ya Mambo ya Nje ya Brazili imetangaza kuwa iko katika "hatua za mwisho" za kuwasilisha mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ uamuzi wa kujiunga na kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya utawala wa kizayuni wa Israel kwa kuhusika na mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Ghaza.
-
Russia yatoa sharti la kufanyika mkutano wa ana kwa ana kati ya Putin na Zelensky
Jul 24, 2025 03:12Kiongozi mkuu wa ujumbe wa Russia katika mazungumzo na Ukraine, Vladimir Medinsky amesema, viongozi wa nchi hizo mbili inapasa wakutane baada ya mkataba wa amani kuwa tayari kutiwa saini, si vinginevyo.
-
Umoja wa Mataifa wahimiza usuluhishi wa amani wa migogoro
Jul 23, 2025 23:18Nchi 193 za Umoja wa Mataifa zimehimizwa kuongeza nguvu zaidi katika usuluhishi wa amani wa migogoro duniani.
-
Utafiti: Bei za vyakula yaathiriwa pakubwa na mabadiliko ya tabianchi
Jul 23, 2025 23:17Imeelezwa kuwa, bei za vyakula imeathiriwa mno na mabadiliko ya tabia nchi.
-
Kwa nini Marekani imejiondoa rasmi UNESCO?
Jul 23, 2025 05:28Marekani ilitangaza Jumanne, Julai 22, kwamba imejiondoa rasmi katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO.
-
Marekani yajitoa tena katika UNESCO kwa sababu ya Palestina
Jul 23, 2025 03:51Marekani imeamua kujiondoa katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa mara ya pili kwa sababu ya uamuzi uliochukuliwa na shirika hilo la UN wa kuikubali Palestina kuwa nchi mwanachama.
-
Uingereza yadokeza kuwa itachukua hatua zaidi dhidi ya Israel kutokana na hali ya 'kikatili' ya Ghaza
Jul 23, 2025 02:41Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy ameonya kuwa ikiwa usitishaji vita katika Ukanda wa Ghaza hautafikiwa hivi karibuni, zinaweza kuchukuliwa hatua zaidi dhidi ya Israel.
-
Mafaili ya siri yanayohusu mauaji ya Martin Luther King Jr yawekwa hadharani
Jul 23, 2025 00:18Serikali ya Rais wa Marekani Donald Trump imeweka hadharani maelfu ya mafaili na nyaraka za serikali zinazohusiana na mauaji ya nyota wa kupigania haki za kiraia Martin Luther King Jr. Siku ya Jumatatu, kurasa zipatazo 240,000 ziliwekwa kwenye tovuti ya Hifadhi ya Taifa, ambayo imeahidi kutoa nyaraka nyingi zaidi.
-
Mkuu wa Sera za Nje wa EU: Machaguo yote dhidi ya Israel yako mezani
Jul 23, 2025 00:10Kaja Kallas, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X akisema: Mauaji ya watu wasio na ulinzi wa Palestina yanapasa kusitishwa; vinginevyo machaguo yote yako mezani.