-
Zaidi ya mabalozi 206 wa zamani wa EU wataka Israel ichukuliwe hatua kali
Aug 26, 2025 22:58Zaidi ya mabalozi 200 wa zamani wa Umoja wa Ulaya na maafisa wa ngazi ya juu jana Jumanne waliituhumu Brussels kwa kushindwa kuchukua hatua za kukabiliana na hali mbaya ya binadamu katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.
-
Je, kustawishwa ushirikiano wa Russia na India ni jibu kwa sera ya mashinikizo ya Trump?
Aug 26, 2025 22:51Sambamba na mashinikizo ya utawala wa Trump dhidi ya India ili ipunguze uhusiano wake na Russia, Waziri wa Mambo ya Nje wa India alisafiri hadi Moscow na kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Russia Vladimir Putin.
-
Mgombea wa chama cha Republican achoma Qur'ani ili kuunga mkono kampeni yake ya uchaguzi
Aug 26, 2025 11:45Mgombea wa chama cha Republican wa kiti cha Kongresi huko Texas, anayejulikana kwa uadui wake mkubwa dhidi ya Waislamu amewakasirisha Waislamu zaidi ya bilioni mbili duniani kwa kuchoma moto nakala ya kitabu hicho kitakatifu ili kuunga mkono kampeni yake ya uchaguzi.
-
Mwandishi habari ajiuzulu Reuters akilalamikia hatua ya shirika hilo kuhalalisha mauaji ya Israel dhidi ya waandishi habari
Aug 26, 2025 11:44Mpiga picha wa Canada, Valerie Zink, ametangaza kujiuzulu kutoka kwenye shirika la habari la Reuters, akipinga nafasi ya shirika hilo katika kuendeleza propaganda za Israel na kuhalalisha mauaji ya waandishi wa habari wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
-
UN, OIC, EU, RSF na hata waitifaki wa Israel walaani shambulio la kinyama lililoua wanahabari Ghaza
Aug 26, 2025 00:09Taasisi za kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC, Umoja wa Ulaya, Shirika la Wanahabari Wasio na Mipaka (RSF) na hata nchi kadhaa za Magharibi waitifaki wa utawala wa kizayuni wa Israel zimelaani vikali shambulio la kinyama lililofanywa na jeshi la utawala huo katika Hospitali ya Nasser iliyoko Khan Younis katika Ukanda wa Ghaza.
-
Norway yalaani jinai za Israel Ukanda wa Gaza
Aug 25, 2025 23:17Norway imeutaja ukatili unaofanya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza kuwa ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, na kutangaza kwamba nchi hiyo ya Ulaya inafikiria kupiga marufuku makampuni ya Norway kushiriki katika shughuli zinazounga mkono upanuzi wa vitongoji vya walowezi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
EU yasisitiza kuiunga mkono "kwa dhati" ICC baada ya US kuwawekea vikwazo waendesha mashtaka 2
Aug 25, 2025 03:08Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema "amesikitishwa sana" na uamuzi wa Marekani wa kuwawekea vikwazo maafisa wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
-
Ufaransa 'yamjia juu' balozi wa US Paris kwa kuituhumu kuwa inahatarisha maisha ya Mayahudi
Aug 25, 2025 03:08Ufaransa imemwita balozi wa Marekani nchini humo Charles Kushner, baada ya mwanadiplomasia huyo kumwandikia barua Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akidai kwamba Paris imeshindwa kuchukua hatua za kutosha kukomesha vitendo vya mabavu dhidi ya Mayahudi raia wa nchi hiyo.
-
UN: Mzozo wa Rohingya umezidi kuwa mbaya kwa zaidi ya miaka minane sasa
Aug 24, 2025 08:22Miaka minane baada ya Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Mynmar kulazimika kuhama katika Jimbo la Rakhine, Umoja wa Mataifa umesema kuwa mzozo unaowakabili raia hao umezidi kuwa mbaya.
-
Russia yatungua droni ya Ukraine iliyokusudia kushambulia kinu cha nyuklia cha Kursk
Aug 24, 2025 07:23Vikosi vya ulinzi wa anga vya Russia vimeitungua ndege isiyo na rubani ya Ukraine (Droni) iliyokuwa imekusudia kutekeleza shambulizi katika kiwanda cha nguvu za nyuklia cha Kursk cha Russia (KNPP).