-
Tel Aviv yakumbwa na mshtuko baada ya Trump kutangaza ushuru kwa bidhaa zote za Israel
Apr 03, 2025 08:03Maafisa wa utawala ghasibu wa Israel wamepatwa na mshtuko baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kutoza ushuru wa asilimia 17 kwa bidhaa zote za Israel, licha ya hivi majuzi Tel Aviv kuondoa ushuru wote kwa bidhaa za Marekani.
-
Baraza la Usalama kufanya mkutano wa dharura kujadili Gaza
Apr 03, 2025 03:36Algeria imeomba kufanyika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili hali ya Palestina. Mkutano huo unatazamiwa kufanyika leo Alkhamisi.
-
Trump atafakari pendekezo la mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Iran
Apr 02, 2025 23:05Ikulu ya Marekani White House inatathmini pendekezo la kufanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Iran; na wakati huo huo inaongeza kiwango cha vikosi vya jeshi lake vamizi katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) ili kujiandaa kwa operesheni tarajiwa za kijeshi dhidi ya Tehran.
-
Russia: Tuko tayari kuunga mkono uhuru wa kidijitali wa Afrika
Apr 02, 2025 23:01Russia imesema iko tayari kupiga jeki nchi za Afrika katika kuendeleza teknolojia zinazohakikisha kuwa kuna utoshelevu na zinaheshimu mamlaka ya kujitawala nchi za bara hilo.
-
Marekani inapokosa mwamana; Trump atishia kuiteka kijeshi Greenland
Apr 02, 2025 09:13Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa ana yakini eneo la Greenland la Denmark kwa vyovyote vile litatekwa na kukaliwa na Marekani hata kama ni kwa kutumia nguvu za kijeshi.
-
Seneta wa US avunja rekodi ya hotuba ndefu, ahutubia kwa saa 25 kukosoa sera za Trump
Apr 02, 2025 07:01Seneta wa Marekani Cory Booker amevunja rekodi iliyodumu kwa miaka 68 ya hotuba ndefu zaidi kutolewa katika historia ya Seneti hiyo alipozungumza kwa zaidi ya saa 25 kupinga na kukosoa sera za rais wa nchi hiyo Donald Trump.
-
Amnesty International: Netanyahu anapaswa kukamatwa na kupelekwa The Hague
Apr 01, 2025 23:36Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetangaza kuwa, mwaliko wa Hungary kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kuzuru nchi hiyo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa, na Budapest inapaswa kumkamata na kumkabidhi kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
-
Wacanada waanza "kumtia adabu" Trump, bidhaa za Marekani zasusiwa Canada
Apr 01, 2025 23:01Kuongezeka himaya na uungaji mkono wa Wacanada kwa bidhaa za nyumbani kumeibua wasiwasi kwa makampuni ya bidhaa mbalimbali ya Marekani.
-
Russia nayo yaionya Washington kuhusu shambulio lolote dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran
Apr 01, 2025 23:00Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameonya kwamba shambulio lolote dhidi ya miundombinu ya nyuklia ya Iran linaweza kuwa na madhara makubwa kwa eneo zima la Mashariki ya Kati.
-
China haitakubali sera ya ‘Marekani Kwanza’ yenye msingi wa ubabe wa Kimarekani
Apr 01, 2025 04:13Waziri wa Mambo ya Nje wa China amesema kuwa sera ya Rais Donald Trump ya ‘Marekani Kwanza’ haiwezi kufanikishwa kwa kutumia mbinu za ubabe wa Kimarekani, hasa iwapo jambo hilo ni kwa hasara ya maslahi ya nchi nyingine.