-
Mwanamke anayechukia Waislamu apatikana na hatia ubadhirifu Ufaransa
Mar 31, 2025 23:10Mahakama moja nchini Ufaransa jana Jumatatu ilimpata na hatia ya ubadhirifu, Marine Le Pen, aliyekuwa mgombea urais wa Ufaransa kwa mihula miwili na kiongozi wa chama cha National Rally (RN) chenye chuki dhidi ya Waislamu. Hukumu hiyo itaathiri mustakabali wake wa kisiasa, hasa kugombea katika uchaguzi wa rais wa Ufaransa wa 2027.
-
Jaribio la kwanza la kurusha roketi anga za juu barani Ulaya lafeli
Mar 31, 2025 08:10Roketi la anga za juu la Ulaya limelipuka muda mfupi tu baada ya kuzinduliwa.
-
Ripoti: Wamarekani wanahamia Mexico kukwepa sera za kibaguzi za Trump
Mar 31, 2025 07:52Katika jitihada za kukwepa siasa na sera za Rais Donald Trump wa chama cha Republican, Wamarekani, baadhi yao wakiwa na asili ya Mexico, wanahamia nchi jirani ya Mexico, katika kile kinachoweza kutambuliwa kuwa uhamiaji wa kinyume.
-
Waziri Mkuu wa Greenland amjibu Trump: Marekani haitakipata kisiwa hiki
Mar 31, 2025 03:28Waziri Mkuu wa Greenland amejibu matamshi ya Rais wa Marekani aliyedai kwamba Washington inataka kukidhibiti kisiwa hicho kikubwa cha ncha ya kaskazini ya dunia, na kusisitiza kwamba: "Marekani haitaipata Greenland".
-
Mamia ya Waislamu wahofiwa kufariki katika tetemeko la ardhi Myanmar
Mar 30, 2025 23:10Mamia ya Waislamu wanahofiwa kuwa miongoni mwa watu zaidi ya 1,600 waliopoteza maisha katika tetemeko kubwa la ardhi lililotokea katikati ya Myanmar, wakati walipokuwa wakiswali misikitini katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Marekani, Mshirika Asiyeaminika
Mar 30, 2025 23:09Waziri Mkuu wa Canada, Mark Carney, ambaye amemrithi Justin Trudeau, amesisitiza kwamba atajibu hatua za Marekani dhidi ya nchi hiyo katika nyanja za kiuchumi na kibiashara, na amekiri kwamba: "Marekani si mshirika wa kuaminika tena."
-
Kuongezeka hatua za Trump dhidi ya vyuo vikuu na wanafunzi wanaowatetea Wapalestina
Mar 30, 2025 03:35Katika muhula wake wa pili wa urais, Donald Trump, rais mpya wa Marekani kwa mara nyingine tena ameamua kutumia mtindo alioutumia katika muhula wake wa kwanza wa kuuunga mkono bila mpaka utawala wa Kizayuni wa Israel na kuchukua hatua mpya za kuisaidia na kuihami Israel dhidi ya Wapalestina.
-
Wanachuo 300 wapokonywa viza US kwa kuiunga mkono Palestina
Mar 30, 2025 02:59Marekani imebatilisha viza za wanafunzi zaidi ya 300 wa kigeni kwa kuratibu na kushiriki katika maandamano ya kuwanga mkono na kuwatetea wananchi madhulumu wa Palestina katika mabewa ya vyuo vikuu kote nchini humo.
-
Baadhi ya Waislamu waswali Iddi leo, wengine kuadhimisha sikukuu hii kesho
Mar 30, 2025 02:42Baadhi ya Waislamu katika maeneo tofauti duniani wameswali Swala ya Iddul-Fitri leo Jumapili, baada ya kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa siku 29; huku wengine wakitazamiwa kuadhimisha sherehe hizo kesho Jumatatu.
-
China: Tuko tayari kustawisha uhusiano wa kijeshi na Iran na Russia
Mar 29, 2025 23:08Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China amezungumzia mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyofanywa na majeshi ya Wanamaji ya nchi hiyo, Iran na Russia na kusisitiza kuwa Beijing iko tayari kustawisha ushirikiano wa kijeshi na nchi hizo mbili.