-
Bajeti ya NATO; changamoto nyingine kwa waitifaki wa pande mbili za Antlantiki
Jan 10, 2025 23:26Baada ya Donald Trump kutaka kuunganishwa Canada, Mfereji wa Panama na eneo la Greenland na ardhi ya Marekani, sasa suala la kuongeza bajeti ya nchi wanachama wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) ni changamoto kuu zaidi inayowatatiza washirika wa pande zote mbili za Bahari ya Atlantiki.
-
Katika hatua ya kuaibisha, Baraza la Wawakilishi la US lapitisha muswada wa vikwazo dhidi ya ICC
Jan 10, 2025 08:42Katika hatua ya kuaibisha, Baraza la Wawakilishi la Marekani limeidhinisha mswada wa kuwawekea vikwazo maafisa wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kama jibu kwa hatua ya mahakama hiyo ya kutoa hati za kukamatwa viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuhusika na uhalifu wa kivita katika Ukanda wa Ghaza.
-
Moto wa nyika wa Los Angeles wateketeza miundo 10,000 huku moto mwingine mpya ukisambaa
Jan 10, 2025 06:59Mioto miwili ya nyika iliyozuka katika eneo la Los Angeles nchini Marekani imeua watu wasiopungua 10 na kuteketeza miundo zikiwemo nyumba na majengo yapatayo 10,000, huku moto mwingine wa tatu ukilazimisha maelfu mengine ya watu kuhama makazi yao.
-
Makomandoo wa UK wafichua: Kikosi maalumu kilipewa 'kibali cha dhahabu' cha kuulia raia Afghanistan
Jan 10, 2025 06:53Askari wa zamani wa jeshi la Uingereza ameiambia tume ya uchunguzi kuwa makomandoo wa kikosi maalumu cha nchi hiyo walikuwa na sera waliyowekewa ya kuua raia bila kujali wakati wa mashambulizi waliyokuwa wakifanya dhidi ya Taliban nchini Afghanistan.
-
Rais wa Mexico apendekeza kubadilishwa jina la Marekani kuwa "Mexican America"
Jan 09, 2025 22:56Rais wa Mexico, Claudia Sheinbaum Pardo, amekosoa matamshi yaliyotolewa na rais mteule wa Marekani, Donald Trump, kuhusu kubadili jina la Ghuba ya Mexico kuwa "Ghuba ya Marekani", akipendekeza jina la Marekani libadilishwe na kuwa "Marekani ya Mexico".
-
Majibu ya nchi mbalimbali kwa madai yasiyo na msingi ya Trump kuhusu kuinyakua Greenland
Jan 09, 2025 09:23Baada ya Rais mteule wa Marekani, Donald Trump kusisitiza madai yake ya kutaka kunyakua maeneo Canada, Panama na Greenland, na hatua zake, ikiwa ni pamoja na kumtuma mtoto wake wa kiume huko Greenland kuandaa mazingira ya unyakuzi huo, nchi hizo zimetoa majibu makali dhidi ya hatua ya Trump.
-
Viongozi wa EU watoleana mwito kuungana dhidi ya kitisho cha Trump cha kuinyakua Greenland
Jan 09, 2025 03:22Viongozi wa nchi za Ulaya wamemuonya Donald Trump dhidi ya hatua yake ya kutishia "mipaka huru" baada ya rais huyo mteule wa Marekani kukataa kufutilia mbali uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi za kuiteka Greenland.
-
Nyota wa zamani wa NBA: Nililazimishwa kufuta haraka mtandaoni ujumbe wa "Palestina Huru"
Jan 09, 2025 02:39Nyota wa zamani wa Ligi ya Mpira wa Vikapu nchini Marekani NBA Dwight Howard amesema, miaka michache iliyopita alilazimika kufuta haraka ujumbe alioweka kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter wa kuunga mkono Palestina.
-
WHO yautoa hofu ulimwengu kuhusu virusi vya HMPV
Jan 08, 2025 23:50Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa ongezeko lililoripotiwa la wagonjwa walioathirika katika mfumo wao wa kupumua linalosababishwa na virusi vya Human Metapneumovirus (hMPV) huko China linaendana na mwelekeo wa msimu wa magonjwa ya kawaida ya kupumua, pamoja na mafua ambayo kwa kawaida hufikia kileleni wakati wa miezi ya baridi.
-
Kuongezeka mapato ya makampuni ya silaha duniani: Marekani inaongoza katika biashara hiyo ya mauaji
Jan 08, 2025 23:49Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI) imetangaza katika ripoti yake kwamba kulikuwepo ongezeko la mapato ya makampuni ya silaha duniani mwaka 2023.