-
Ufaransa yamuonya Trump kuhusu eneo la Greenland la Denmark
Jan 08, 2025 23:41Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Noel Barrot, jana Jumatano alimtahaharisha Donald Trump kuhusu hatua yake ya kutishia "mipaka huru" ya Umoja wa Ulaya baada ya rais huyo mteule wa Marekani kukataa kutupilia mbali hatua za kijeshi za kutaka kuidhibiti Greenland, eneo linalojitawala la mwanachama wa Umoja wa Ulaya, Denmark.
-
Jibu la Mexico kwa "Trump": Jina la Ghuba ya Mexico halitabadilika
Jan 08, 2025 08:50Mexico imeji madai ya Donald Trump na kumwambia wazi kwamba jina la Ghuba ya Mexico kamwe halitobadilika na kuwa "Ghuba ya Amerika."
-
CNN: Hofu ya kukamatwa katika mataifa mengine inawatia kiwewe wanajeshi wa Israel
Jan 07, 2025 04:08Televisheni ya CNN ya Marekani imetangaza katika ripoti yake kuwa kufuatia malalamiko ya mahakama ya Brazil dhidi ya mwanajeshi wa Israel anayekabiliwa na tuhuma za kutenda jinai za kivita, askari wa utawala wa Kizayuni wanakabiliwa na hatari ya kukamatwa na kufunguliwa mashtaka katika nchi nyingine, jambo ambalo limezua taharuki miongoni mwa maafisa wa serikali ya Tel Aviv.
-
Ripoti: Uhalifu wa kibaguzi umevunja rekodi nchini Ujerumani
Jan 07, 2025 02:41Ujerumani imerekodi zaidi ya uhalifu 33,000 wa kibaguzi mwaka uliomalizika majuzi wa 2024, ambayo ni rekodi isiyo na kifani tangu mwanzo wa kusajili uhalifu huo mnamo 2001.
-
Zaidi ya Warohingya 200 wakimbilia pwani ya Indonesia kwa boti mbovu
Jan 06, 2025 23:12Zaidi ya Warohingya 200 wamewasili kwenye ufuo wa mkoa wa Aceh nchini Indonesia, katika wimbi jipya la kuhama makwao Waislamu hao walio wachache nchini Myanmar ambao wanakabiliwa na mateso na mauaji ya kimbari.
-
Australia yajitoa kuandaa Kombe la Dunia kwa hofu ya maandamano ya kuunga mkono Palestina
Jan 06, 2025 23:11Australia ambayo ilikuwa iandae mashindano ya Kombe la Dunia ya mchezo wa Hoki ya Barafu imejitoa ikihofia kufanyika maandamano dhidi ya Israel katika nchi yake wakati wa kufanyika mashindano hayo.
-
Onyo kuhusu athari za kiusalama za mpasuko wa anga ya kisiasa ya Marekani
Jan 06, 2025 23:10Tovuti ya mtandao wa televisheni ya Marekani NBC imeandika katika ripoti yake kuhusu suala la kushamiri itikadi kali katika anga ya mtandaoni, ikionya kuhusu madhara ya usalama ya mpasuko wa nga ya kisiasa ya Marekani.
-
Je, unajua pombe huua maelfu mangapi ya Wamarekani kila mwaka?
Jan 06, 2025 09:51Daktari Mkuu wa Upasuaji wa Marekani anaripoti kwamba maelfu ya Wamarekani hufariki dunia kila mwaka kutokana na unywaji pombe.
-
Mamilioni wakumbwa na baridi kali Marekani; zaidi ya safari 2,000 za ndege zaakhirishwa
Jan 06, 2025 09:34Hali hatari sana ya hewa ya baridi imekumba eneo kubwa la kati kati mwa Marekani, huku dhoruba kali ikielekea upande wa mashariki, na kusababisha usumbufu kwa usafiri na kazi kutoka Kansas City hadi Washington DC.
-
Gazeti la The Times: Uingereza inahujumika kirahisi kwa makombora ya balestiki
Jan 06, 2025 02:34Gazeti la The Times linalochapishwa London, Uingereza limezinukuu duru za ulinzi na kuripoti kuwa, "matundu" yaliyopo katika ulinzi wa anga wa nchi hiyo yanaitia wasiwasi Uingereza yenyewe na wanachama wengine wa shirika la kijeshi la NATO, kwa kuwepo uwezekano wa kuhujumika kirahisi nchi hiyo kwa mashambulizi ya makombora ya balestiki.