Jibu la Mexico kwa "Trump": Jina la Ghuba ya Mexico halitabadilika
https://parstoday.ir/sw/news/world-i121170-jibu_la_mexico_kwa_trump_jina_la_ghuba_ya_mexico_halitabadilika
Mexico imeji madai ya Donald Trump na kumwambia wazi kwamba jina la Ghuba ya Mexico kamwe halitobadilika na kuwa "Ghuba ya Amerika."
(last modified 2025-01-08T08:50:00+00:00 )
Jan 08, 2025 08:50 UTC
  • Jibu la Mexico kwa

Mexico imeji madai ya Donald Trump na kumwambia wazi kwamba jina la Ghuba ya Mexico kamwe halitobadilika na kuwa "Ghuba ya Amerika."

Marcelo Ebrard, Waziri wa Uchumi wa Mexico amesema mbele ya waandishi wa habari leo Jumatano na kusema kuwa njama za Trump za kutaka kubadilisha historia hazitofanikiwa. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico amesisitiza kuwa: "Ikiwa tutaangalia katika miaka 30, Ghuba ya Mexico muda wote imekuwa ikiitwa Ghuba ya Mexico, hatutaingia katika mjadala huu. Tunachotaka kufanya ni kulinda uhusiano kati ya nchi hizo mbili."

Hapo awali, akijibu vitisho vya Trump vya kutoza ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Mexico, Marcelo Ebrard amesisitizia haja ya kudumishwa utulivu na akatangaza kwamba Mexico ni nchi huru na haifai kuathiriwa na chokochoko za rais mteule wa Marekani.