Je, unajua pombe huua maelfu mangapi ya Wamarekani kila mwaka?
Daktari Mkuu wa Upasuaji wa Marekani anaripoti kwamba maelfu ya Wamarekani hufariki dunia kila mwaka kutokana na unywaji pombe.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Marekani, Vivek Murthy, ameonya kuhusu takwimu za kutisha za vifo vinavyosababishwa na unywaji pombe katika jamii ya Marekani na kuisema: Pombe ni chanzo cha nne cha vifo nchini Marekani, na zaidi ya watu 140,000 hufarikii dunia kwa wastani kila mwaka kutokana na unywaji pombe.
Jumuiya ya Saratani ya Marekani hapo awali ilitangaza kwamba kiwango chochote cha unywaji pombe, hata kiasi kidogo, kinaweza kusababisha aina sita za saratani.
Taasisi ya Kitaifa ya Unywaji na Uraibu wa Pombe ya Marekani imetangaza katika ripoti ya kushangaza kwamba watu 100,000 hupata saratani kila mwaka kutokana na unywaji wa vileo na kusisitiza kwamba: Uchanganuzi wa vyeti vya vifo katika miaka iliyopita ulionyesha kwamba vifo vinavyotokana na pombe nchini Marekani vimeongezeka kwa asilimia 26.