-
Seneta wa Marekani aunga mkono hati ya ICC inayoamuru kukamatwa Netanyahu na Gallant
Nov 22, 2024 04:10Seneta wa Marekani Bernie Sanders ameunga mkono uamuzi uliotoloewa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC jana Alkhamisi wa kuamuru kukamatwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa zamani wa vita wa utawala huo haramu Yoav Gallant.
-
Putin aonya kujibu mapigo kwa nchi zinazotoa silaha za kushambulia ardhi ya Russia
Nov 22, 2024 03:54Rais Vladimir Russia ameonya kuwa, Moscow inabaki nayo haki yake ya kushambulia vituo vya kijeshi vya nchi zinazoruhusu silaha zao kutumika dhidi ya ardhi ya nchi hiyo.
-
Magaidi wakufurishaji waua Waislamu 40 wa Kishia, wajeruhi 30 kaskazini magharibi mwa Pakistan
Nov 22, 2024 02:58Kundi la magaidi wakufurishaji limeyafyatulia risasi magari ya abiria yaliyokuwa yamebeba raia Waislamu wa madhehebu ya Shia kaskazini-magharibi mwa Pakistan na kuua karibu watu 40 na kujeruhi wengine 30 katika moja ya mashambulizi mabaya zaidi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni kwenye eneo hilo lenye machafuko.
-
Hata Uholanzi, Canada na Uswisi zasema zitamkamata Netanyahu akithubutu kutembelea nchi hizo
Nov 22, 2024 02:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi amekaribisha uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC wa kutoa hati ya kukamatwa Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema kwamba iwapo ataingia Uholanzi atatiwa nguvuni.
-
Borrell: Hati ya kukamatwa Netanyahu, Gallant si ya kisiasa, nchi zote za EU zina wajibu wa kuitekeleza
Nov 21, 2024 23:59Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell amesema, hati zilizotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC za kuamuru kukamatwa waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa zamani wa vita wa utawala huo Yoav Gallant si maamuzi ya "kisiasa" na ni lazima "yaheshimiwe" na nchi zote wanachama wa umoja huo.
-
Siku ya Kimataifa ya Watoto Duniani na siku za huzuni kwa watoto wa Gaza na Lebanon
Nov 21, 2024 08:59Siku ya Kimataifa ya Watoto imeadhimishwa duniani huku mauaji ya watoto wa Gaza na Lebanon yanayofanywa na utawala wa Kizayuni yakiendelea bila huruma, suala ambalo pia limeibua wasiwasi kwa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF.
-
Marekani yapinga tena azimio la kusitisha mapigano Gaza
Nov 21, 2024 07:27Ikiwa ni katika muendelezo wa uungaji mkono wake mkubwa kwa utawala ghasibu wa Israel, mapema siku ya Jumatano Novemba, Marekani ilipinga tena rasimu ya azimio la wanachama 10 wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lililotaka usitishaji vita wa mara moja, usio na masharti na wa kudumu huko Gaza na kuachiliwa huru mateka wote.
-
Marekani yapinga tena rasimu ya azimio la kusitisha vita, Gaza
Nov 21, 2024 04:22Katika kuuhami na kuunga mkono utawala wa Israel, Marekani kwa mara nyingine tena imelipigia kura ya turufu azimio la nchi 10 wanachama wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zilizotaka kutekelezwa usitishwaji vita haraka iwezekanavyo, bila ya masharti na wa kudumu katika Ukanda wa Gaza na kuachiwa mateka wote.
-
Nchi za Kiislamu zichukue hatua dhidi ya askari wa Israel aliyevunjia heshima Qur'ani
Nov 21, 2024 00:20Kitendo cha hivi punde zaidi cha kuvunjiwa heshima Qur'ani na askari wa utawala haramu wa Israel huko Gaza kimelaaniwa na watu wengi, ikiwa ni pamoja na kundi kubwa zaidi la kutetea Waislamu nchini Marekani ambalo lilitaka Waislamu wachukuliwe hatua dhidi ya hatua hizo za kusikitisha.
-
Kamanda wa Marekani akiri kusalia matupu maghala ya silaha ya nchi hiyo
Nov 20, 2024 08:36Kamanda wa jeshi la Marekani katika eneo la Indo- Pacific amekiri kuwa maghaala ya silaha ya nchi hiyo hivi sasa yapo matupu.