-
Mahakama ya ICT Bangladesh yamhukumu adhabu ya kifo waziri mkuu wa zamani Hasina
Nov 17, 2025 07:18Baraza la Mahakama la Jinai za Kimataifa (International Crimes Tribunal), ICT la Bangladesh leo limetoa hukumu ya adhabu ya kifo kwa Waziri Mkuu wa zamani aliyeitoroka nchi Sheikh Hasina, baada ya kumpata na hatia ya kuhusika na jinai dhidi ya binadamu-mbali na makosa mengine-, kwa uhalifu uliofanywa mwaka jana wakati wa maandamano makubwa zaidi kuwahi kutokea ya kupinga serikali yake.
-
Katika kura ya maoni, Waecuador wakataa US kuwa na kituo cha kijeshi tena nchini mwao
Nov 17, 2025 07:17Wananchi wa Ecuador wamekataa pendekezo la kuruhusu kurejeshwa tena nchini humo vituo vya kijeshi vya nchi za kigeni. Hayo ni kwa mujibu wa matokeo ya awali ya kura ya maoni, ambapo hesabu za asilimia 90 ya kura zinaonyesha kuwa karibu theluthi mbili ya walioshiriki wamepiga kura ya “hapana” kupinga pendekezo hilo.
-
Silaha za Australia zinatumika katika mauaji ya kimbari Sudan?
Nov 16, 2025 23:18Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), unaoshutumiwa kwa kuunga mkono waasi wa RSF wanaotekeleza ukatili na mauaji ya kimbari Sudan, umeibuka kuwa soko kubwa zaidi la silaha za Australia.
-
Pep Guardiola awataka Wahispania kushikamana na Palestina
Nov 16, 2025 03:39Kocha wa Manchester City Mhispania Pep Guardiola, amewataka wananchi wa Uhispania kuonyesha mshikamano na wananchi wa Palestina.
-
Nchi wanachama wa NATO kuilipa Marekani yuro milioni 400 za silaha itakazoipatia Ukraine
Nov 15, 2025 22:57Katibu Mkuu wa shirika la kijeshi la NATO Mark Rutte amesema, nchi kadhaa wanachama wa shirika hilo zitachangia kwa pamoja shehena ya silaha na zana za kijeshi yenye thamani ya yuro milioni 400 kwa ajili ya Ukraine, ambazo zitanunuliwa kutoka Marekani.
-
Kwa nini China na Russia zimepinga azimio lililopendekezwa na Marekani kuhusu Gaza?
Nov 15, 2025 22:56Russia na China ambazo ni wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zimetaka kufutwa kikamilifu "Tume ya Amani" kwenye matini ya rasimu iliyowasilishwa na Marekani kwenye baraza kuhusu Gaza.
-
Sababu za Trump kuyaweka kwenye orodha ya "ugaidi wa kimataifa" makundi manne ya mrengo wa kushoto ya Ulaya
Nov 15, 2025 09:15Washington imeyaweka kwenye orodha ya "ugaidi wa kimataifa" makundi manne ya mrengo wa kushoto yenye misimimamo mikali ya barani Ulaya.
-
Trump ajisalimisha kwa mfumuko wa bei; Marekani kupunguza ushuru kwa baadhi ya nchi za Amerika ya Kusini
Nov 15, 2025 07:46Ongezeko la bei za baadhi ya bidhaa za kimsingi nchini Marekani limeilazimisha serikali kujizuia kutoza ushuru wa ziada kwa uagizaji wa baadhi ya bidhaa kutoka Amerika Kusini.
-
Kwa nini Marekani inataka Uturuki iachane na nishati ya Russia?
Nov 14, 2025 23:08Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameitaka Uturuki iache kununua nishati ya Russia.
-
Iran yalaani jinai zinazotendwa nchini Sudan
Nov 14, 2025 23:06Iran imepaza sauti kulaani “jinai na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu” unaoendelea nchini Sudan, ikisisitiza kuwa hali ya kibinadamu katika mji wa Al-Fasher na maeneo jirani imefikia kiwango cha hatari kinachohitaji msaada wa haraka wa jumuiya ya kimataifa.