-
UN yakosoa mashambulizi ya Marekani dhidi ya meli zinazoshukiwa kubeba dawa za kulevya
Oct 31, 2025 23:03Umoja wa Mataifa jana Ijumaa ulitoa wito kwa Washington kusimamisha mashambulizi yake dhidi ya meli na boti katika Bahari ya Karibi na mashariki mwa Pasifiki zinazotuhumiwa na Washington kuwa zinafanya biashara haramu ya dawa za kulevya, na kukomesha mauaji yanayofanywa kinyume cha sheria.
-
Mwanamfalme wa Uingereza avuliwa vyeo vyote vya kifalme na kufukuzwa nyumbani kwake
Oct 31, 2025 23:03Katika matokeo ya hivi karibuni ya kashfa ya Jeffrey Epstein, Kasri ya Mfalme wa Uingereza, Buckingham Palace, ilitangaza jana Ijumaa kwamba Andrew, kaka wa mfalme wa Uingereza, atajulikana kama Andrew Mountbatten Windsor na si Mwanamfalme, na hatakuwa tena na haki ya kutumia vyeo vyake vyovyote vya kifalme.
-
Kwa nini Iran inataka kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Cuba bila masharti yoyote?
Oct 31, 2025 09:15Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo vyote dhidi ya Cuba bila masharti yoyote.
-
Marekani yahamaki vibaya kwa kushindwa kuipokonya silaha Hizbullah
Oct 31, 2025 03:22Viongozi wa Marekani wameshindwa kuficha hamaki zao kutokana na kufeli njama zao zote za kuipokonya silaha harakati ya Muqawama na mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon. Wameonesha hamakii zao katika mahojiano na televisheni moja ya lugha ya Kiarabu baada ya kuona serikali ya Lebanon imeshindwa kuipokonya silaha Hizbullah licha ya njama zao za usiku na mchana.
-
Madai yasiyo na msingi ya Trump ya eti ushindi wa Marekani katika vita vyote; ni kujisahaulisha matukio ya Afghanistan na Iraq?
Oct 30, 2025 23:43Rais wa Marekani, Donald Trump, amedai kwamba nchi hiyo itashinda kama itaingia vitani na nchi yoyote.
-
Trump aiamuru Wizara ya Vita ya Marekani kuanza tena majaribio ya silaha za nyuklia
Oct 30, 2025 08:47Rais Donald Trump wa Marekani ameiagiza Wizara ya Vita ya nchi hiyo kuanza tena majaribio ya silaha za nyuklia; katika uamuzi ambao umewatia wasiwasi wapinzani wa silaha za maangamizi ya umati na wataalamu masuala ya usalama duniani.
-
Agizo la Trump la kuanza tena majaribio ya silaha za nyuklia; Dunia inarudi kwenye mashindano ya silaha za nyuklia?
Oct 30, 2025 08:22Rais Donald Trump wa Marekani ameamuru kuanzishwa tena majaribio ya silaha za nyuklia za nchi hiyo.
-
Marekani kuunda kikosi kipya cha kijeshi cha kukandamiza raia
Oct 30, 2025 03:17Wizara ya Vita ya Marekani imeamuru wanajeshi wa Gadi ya Taifa kuunda kikosi kipya haraka kwa ajili ya kukandamiza zaidi raia wanaolalamikia uongozi mbovu wa Trump katika majimbo yote ya Marekani. Kikosi hicho kitapewa nguvu zote za kukandamiza maandamano ya wananchi ya kupigania haki zao.
-
Ripota wa UN amfumba mdomo vibaya Mzayuni
Oct 30, 2025 01:26Baada ya mwakilishi wa Israel katika Umoja wa Mataifa kumwita Francesca Albanese, ripota maalumu wa umoja huo katika masuala ya Palestina kuwa ni mchawi, Albanese ametoa majibu makali yaliyomziba mdomo Mzayuni huyo na kumfedhehesha mbele ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
-
Mpango wa siri ulioshindwa: Marekani imejaribu kuajiri rubani wa Maduro ili kumkamata kiongozi wa Venezuela
Oct 29, 2025 22:55Ajenti wa Shirikisho la Marekani alijaribu kumsajili rubani binafsi wa Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, Jenerali Bitner Villegas, katika mpango wa siri, ili kuipeleka ndege ya rais huyo huko Marekani. Hayo yamefichuliwa na shirika la habari la Associated Press.