Marekani yahamaki vibaya kwa kushindwa kuipokonya silaha Hizbullah
https://parstoday.ir/sw/news/world-i132630-marekani_yahamaki_vibaya_kwa_kushindwa_kuipokonya_silaha_hizbullah
Viongozi wa Marekani wameshindwa kuficha hamaki zao kutokana na kufeli njama zao zote za kuipokonya silaha harakati ya Muqawama na mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon. Wameonesha hamakii zao katika mahojiano na televisheni moja ya lugha ya Kiarabu baada ya kuona serikali ya Lebanon imeshindwa kuipokonya silaha Hizbullah licha ya njama zao za usiku na mchana.
(last modified 2025-10-31T10:25:15+00:00 )
Oct 31, 2025 06:52 UTC
  • Marekani yahamaki vibaya kwa kushindwa kuipokonya silaha Hizbullah

Viongozi wa Marekani wameshindwa kuficha hamaki zao kutokana na kufeli njama zao zote za kuipokonya silaha harakati ya Muqawama na mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon. Wameonesha hamakii zao katika mahojiano na televisheni moja ya lugha ya Kiarabu baada ya kuona serikali ya Lebanon imeshindwa kuipokonya silaha Hizbullah licha ya njama zao za usiku na mchana.

Wakihojiwa na televisheni ya lugha ya Kiarabu ya Sky News Arabic, viongozi hao wa Marekani wameshindwa kuficha hamaki na chuki zao kubwa wakidai kuwa serikali ya Lebanon haichukui hatua wanazotaka za kuipokonya silaha Hizbullah na wametoa vitisho dhidi ya Beirut.

Kwa mujibu wa televisheni hiyo ya Sky News, maafisa hao wa serikali ya Marekani wamesema kwamba "Lebanon imekosa fursa ya kufikia suluhisho la kuipokonya silaha Hizbullah na tuna wasiwasi kuwa, kuna jambo baya zaidi litalotokea."

Viongozi hao wa Marekani ambao hawakutajwa majina yao pia wamedai kwamba majaribio ya mara kwa mara ya Washington na nchi za ukanda huu ya kutoa motisha za kiuchumi na kisiasa kwa Lebanon "yamegonga ukuta wa chuma."

Sky News imewanukuu viongozi hao wa Marekani wakiendelea kulalamika kuwa, vyama muhimu nchini Lebanon vinakataa mpango wa kupokonywa silaha Hizbullah.

Hizbullah ni nguvu ya kisiasa na kijeshi ndani na nje ya Lebanon na nguvu zake za kijeshi ndizo zinazoilinda nchi hiyo na chokochoko za maadui hasa utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Harakati hiyo ya Muqawama wa Kiislamu imekuwa ikitangaza muda wote kwamba nguvu zake za kijeshi ni kwa ajili ya kupambana na maadui na kuwalinda wananchi wa Lebanon suala ambalo linawahamanisha maadui wa taifa hilo la Kiarabu wakiongozwa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.