Zaidi ya watoto 22,000 wameuawa katika mashambulizi ya Israel Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i132606-zaidi_ya_watoto_22_000_wameuawa_katika_mashambulizi_ya_israel_gaza
Mkurugenzi wa idara ya magonjwa ya watoto na uzazi katika Kituo cha Tiba cha Nasser huko Gaza amesema leo Alkhamisi kuwa, zaidi ya watoto 22,000 wa Kipalestina wameuawa shahidi katika Ukanda huo tangu kuanza kwa mashambulizi ya utawala wa Israel (Oktoba 2023).
(last modified 2025-10-30T13:59:19+00:00 )
Oct 30, 2025 13:57 UTC
  • Zaidi ya watoto 22,000 wameuawa katika mashambulizi ya Israel Gaza
    Zaidi ya watoto 22,000 wameuawa katika mashambulizi ya Israel Gaza

Mkurugenzi wa idara ya magonjwa ya watoto na uzazi katika Kituo cha Tiba cha Nasser huko Gaza amesema leo Alkhamisi kuwa, zaidi ya watoto 22,000 wa Kipalestina wameuawa shahidi katika Ukanda huo tangu kuanza kwa mashambulizi ya utawala wa Israel (Oktoba 2023).

Ahmed Al-Farah, mkurugenzi wa idara ya magonjwa ya watoto na uzazi katika jengo la Nasser Medical Complex huko Gaza, alitangaza kuwa watoto wengine 5,500 wa Kipalestina wanahitaji kusafirishwa hharaka kwa ajili ya kuupata matibabu ya dharura nje ya Gaza, lakini vizuizi na vivuko vilivyofungwa vimezuia hili.

Mkurugenzi wa idara ya magonjwa ya watoto na uzazi katika jengo la Nasser Medical Complex huko Gaza pia ameongeza kuwa watoto 44 wa Kipalestina wamepoteza maisha hadi sasa kwa sababu tu walizuiwa kuondoka Gaza kwa ajili yya kwenda kupata matibabu nje ya Ukanda huo. Afisa wa afya wa Palestina alielezea hali ya sasa kama "janga kamili la kibinadamu" na kusema kwamba jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua mara moja kuokoa maisha ya watoto waliojeruhiwa na wagonjwa huko Gaza.