Wananchi wa Tanzania wanaendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi
Wananchi wa Tanzania wanaendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi uliofanyika jana Jumatano na kutawaliwa na maandamano ya hapa na pale huku hali ya mambo ikianza kurejea katika hali ya kawaida.
Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania INEC imeanza kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais.
Hadi kufikia sasa ni mikoa minne pekee iliofanikiwa kuwasilisha matokeo yake.
Kulingana na matokeo hayo Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama tawala cha CCM Samia Suluhu Hassan anaongoza kulingana na kura zilizohesabiwa.
Polisi katika mji wa Dar es Salaam nchini Tanzania wamefyatua risasi na vitoa machozi leo kutawanya waandamanaji wachache waliorejea barabarani siku moja baada ya uchaguzi uliogubikwa na maandamano katika baadhi ya maeneo.
Maandamano yalizuka mjini Dar es Salaam na miji mingine kadhaa wakati wa upigaji kura siku ya Jumatano, huku waandamanaji wakilalamikia kukamatwa kwa viongozi wakuu wa upinzani na kuzuiliwa kushiriki katika uchaguzi wa Urais mbali na madai ya ukandamizaji wa wakosoaji wa serikali.
Jana baadhi ya miji kamam Dar es Salaam, Mbeya na Dodoma waliwashambulia walioshiriki katika shughuli ya kupiga kura.
Wakati huo vyombo vya usalama vimetangaza kuwa, waandamanaji wachache waliojitokeza leo katika baadhi ya miji na kufanya uharibifu wamedhibitiwa na hali ya mambo imerejea katika hali kawaida.
Mama Samia Suluhu Hassan ambaye kwa mujibu wa takwimu amefanya mambo mengi katika kipindi alichoongoza akipokea nafasi hiyo kutoka kwa mwqendazake John Pombe Magufuli. Mama Samia anapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi katika uchaguzi uliofanyika jana.
Wakati huo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Thabit Aidarous, amewahakikishia wananchi wa visiwa hivyo kwamba matokeo rasmi ya uchaguzi yatatangazwa rasmi leo .
 
							 
						 
						