-
UN: Janga la njaa la Ghaza ni matokeo ya kucheleweshwa upelekaji misaada kwa miezi 22
Aug 28, 2025 02:37Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na uratibu wa masuala ya kibinadamu ametangaza kuwa baa la njaa lililothibitishwa rasmi katika Ukanda wa Ghaza ni matokeo ya kucheleweshwa kwa miezi 22 upelekaji misaada ya kibinadamu katika eneo hilo la Palestina lililowekewa mzingiro na Israel.
-
Aliyeua watoto kwa bunduki katika skuli ya kanisa Marekani ni mwanamume aliyebadilisha jinsia
Aug 28, 2025 02:36Mshambuliaji aliyefyatulia risasi kanisa katika skuli ya kikatoliki kusini mwa mji wa Minneapolis nchini Marekani jana Jumatano na kuua na kujeruhi watu kadhaa ametambuliwa na gazeti la The New York Post kama Robin Westman. Kwa mujibu wa gazeti hilo, inasemekana Westman alibadilisha jina lake la Robert na kuwa Robin mwaka 2020 na kujitambulisha kama mwanamke.
-
Venezuela yashukuru Iran kwa mshikamano dhidi ya vitisho vya uvamizi vya Marekani
Aug 28, 2025 00:48Waziri wa mambo ya nje wa Venezuela ameishukuru Iran kwa msimamo wake thabiti wa kuunga mkono taif hilo a la Amerika ya Kusini mbele ya vitisho vya uchokozi vinavyotolewa na Marekani.
-
Azma ya Malaysia ya uungaji mkono endelevu kwa Palestina
Aug 28, 2025 00:47Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Malaysia amesema kuwa, nchi hiyo itadhibiti na kusimamia vilivyo vitisho au ugaidi wowote unaohusiana na suala la uungaji mkono wa Kuala Lumpur kwa Palestina na kuwa itadumisha misimamo ya kuwaunga mkono Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni.
-
Mawakili wa Uingereza katika vita vya kisheria dhidi ya Uzayuni
Aug 28, 2025 00:47Dunia imeshuhudia karibu miezi 23 ya mauaji ya wazi dhidi ya watu wa Palestina yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Mjumbe wa Trump akosolewa vikali kwa kuwataka waandishi habari waache "uhayawani"
Aug 27, 2025 07:11Kejeli za matusi ya ubaguzi wa rangi kutoka kwa mjumbe wa kikanda wa Marekani dhidi ya waandishi wa habari wa Lebanon zimezusha wimbi la ukosoaji miongoni mwa watu wengi wanaotembelea mitandao ya kijamii, wakiwemo wanaharakati wanaopinga ukoloni na watu mashuhuri wa Lebanon.
-
Waziri Mkuu wa India 'apuuza' simu 4 za Trump huku vita vya kibiashara vya Marekani vikiendelea
Aug 27, 2025 03:28Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, ameripotiwa kupuuza majaribio kadhaa ya Donald Trump ya kumtafuta kwa simu huku vita vya kibiashara kati ya nchi hizo vikipamba moto, ambavyo vimechochewa na ushuru mzito wa forodha wa rais wa Marekani dhidi ya bidhaa kutoka India.
-
Venezuela yapeleka meli za kivita, ndege zisizo na rubani pwani, wakati kikosi cha wanamaji cha Marekani kikikaribia
Aug 27, 2025 03:27Venezuela imetangaza kuwa imepeleka meli za kivita na ndege zisizo na rubani kwenye eneo lake la maji na kufanya doria kwenye ufuo wa pwani ya nchi hiyo ili kukabiliana na hatua ya Marekani ya kutuma meli kadhaa za kivita katika eneo la Karibea kwa kile ilichodai ni kwa ajili ya kukabiliana na biashara ya madawa ya kulevya na kumshinikiza Rais Nicolás Maduro.
-
Zaidi ya mabalozi 206 wa zamani wa EU wataka Israel ichukuliwe hatua kali
Aug 26, 2025 22:58Zaidi ya mabalozi 200 wa zamani wa Umoja wa Ulaya na maafisa wa ngazi ya juu jana Jumanne waliituhumu Brussels kwa kushindwa kuchukua hatua za kukabiliana na hali mbaya ya binadamu katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.
-
Je, kustawishwa ushirikiano wa Russia na India ni jibu kwa sera ya mashinikizo ya Trump?
Aug 26, 2025 22:51Sambamba na mashinikizo ya utawala wa Trump dhidi ya India ili ipunguze uhusiano wake na Russia, Waziri wa Mambo ya Nje wa India alisafiri hadi Moscow na kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Russia Vladimir Putin.