Venezuela: Netanyahu mtenda jinai anaendelea kuhujumu jitihada za amani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i131626-venezuela_netanyahu_mtenda_jinai_anaendelea_kuhujumu_jitihada_za_amani
Yván Gil Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela amemtaja Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel kama muuaji sugu anayeendelea kuhujumu jitihada za kuhitimisha vita huko Gaza.
(last modified 2025-10-05T10:49:35+00:00 )
Oct 05, 2025 10:49 UTC
  • Venezuela: Netanyahu mtenda jinai anaendelea kuhujumu jitihada za amani

Yván Gil Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela amemtaja Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel kama muuaji sugu anayeendelea kuhujumu jitihada za kuhitimisha vita huko Gaza.

Gil amebainisha haya katika ujumbe aliotuma katika ukurasa wake wa telegramu ambapo amemtaja Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni kuwa ni mtenda jinai na muuaji sugu ambaye anakwamisha jitihada za kurejesha amani zinazoungwa mkono na nchi za Kiarabu na Kiislamu. 

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Venezuela ametaka kuheshimiwa kwa haki zote za wananchi wa Palestina na kufanikishwa njia ya kurejea salamaWapalestina katika ardhi zao kupitia mchakato wa uhakika wa amani. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela ameeleza haya huku Israel ikiendelea kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.  Makumi ya Wapalestina wameuawa shahidi katika mashambulizi mapya yaliyofanywa na Israel tangu jana Jumamosi.  

Ijumaa iliyopita, Hamas ilijibu pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kusitisha vita huko Gaza, na kuafiki baadhi ya nukta za mapendekezo hayo na kutaka kufanyika mazungumzo zaidi kujadili vipengee vingine vya mapendekezo ya Trump.