Baraza la Mawaziri Sudan lafanya kikao cha kwanza mjini Khartoum tangu 2023
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i130046-baraza_la_mawaziri_sudan_lafanya_kikao_cha_kwanza_mjini_khartoum_tangu_2023
Baraza la Mawaziri la Sudan ya Sudan lilifanya mkutano wake wa kwanza katika mji mkuu, Khartoum, jana Jumanne tangu kuzuka kwa vita vya ndani nchini humo katikati ya Aprili, 2023.
(last modified 2025-08-27T06:58:13+00:00 )
Aug 27, 2025 06:58 UTC
  • Baraza la Mawaziri Sudan lafanya kikao cha kwanza mjini Khartoum tangu 2023

Baraza la Mawaziri la Sudan ya Sudan lilifanya mkutano wake wa kwanza katika mji mkuu, Khartoum, jana Jumanne tangu kuzuka kwa vita vya ndani nchini humo katikati ya Aprili, 2023.

Shirika rasmi la Habari la Sudan limeripoti kwamba "Serikali ya Matumaini," inayoongozwa na Waziri Mkuu, Kamil Idris, "ilijadili, katika kikao chake cha kwanza rasmi mjini Khartoum baada ya kuundwa kwake, mipango ya wizara zote kwa mwaka huu, ikizingatia huduma za raia, maisha, usalama wa raia, ujenzi mpya, na kuhakikisha kurudi makwao raia kwa hiari yao."

Idris aliwaambia waandishi wa habari kwamba mkutano huo ulijadili mada kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uchumi wa taifa katika nyanja zake zote, kuandaa mazingira ya kurudi wakiimbizi kwa raia, na kujenga upya kile kilichoharibiwa na vita katika Jimbo la Khartoum.

Waziri Mkuu wa Sudan amesisitiza haja ya kuimarishwa uhusiano wa kigeni, kuzingatia diplomasia rasmi, na kufanya mazungumzo ya kina ya baiina ya Wasudan ili kutatua mgogoro wa sasa.

Mkutano huo unakuja baada ya kutangazwa mpango wa kuhamishia serikali mjini Khartoum mwezi Oktoba au Novemba mwaka huu, kufuatia kipindi kirefu cha kuendesha masuala ya serikali katika mji wa mashariki wa Port Sudan.

Kikao cha Baraza la Mawazirii la serikali ya Sudan mjini Khartoum kinatambuliwa kuwa ni hatua ya kurejeshwa taasisi za serikali katika mji mkuu, huku kukiwa na mipango ya usalama ili kuhakikisha utulivu baada ya mji huo kukombolewa kutoka kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).

Tarehe 21 Mei, jeshi la Sudan lilitangaza kudhibiti kikamili mji wa Khartoum na kuukomboa kutoka kwa waasi wa RSF.