Kukanusha kukaribia kusainiwa makubaliano ya usalama kati ya serikali ya mpito ya Syria na utawala wa Israel
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya serikali ya mpito ya Syria siku ya Jumamosi ilikanusha habari iliyochapishwa kuhusu kukaribia kusainiwa kwa makubaliano ya usalama kati ya Damascus na utawala wa Kizayuni.
Ofisi ya Uratibu na Mawasiliano ya Idara Kuu ya Habari ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Muda ya Syria, ikijibu swali la kanali ya televisheni ya "Syria" kuhusu kukaribia kusainiwa makubaliano ya usalama kati ya Damascus na utawala wa Kizayuni mnamo Septemba 25 katika Umoja wa Mataifa, imesema: 'Habari zilizochapishwa kuhusu suala hili sio sahihi.' Awali, baadhi ya vyombo vya habari vya Kiarabu viliripoti, vikinukuu vyanzo vya juu vya Syria, kwamba "wahusika wanapanga kutia saini makubaliano ya usalama kwa upatanishi wa Marekani, na kuwa kabla ya makubaliano hayo, Ahmad al-Shara, rais wa serikali ya mpito ya Syria, amepangwa kutoa hotuba katika Umoja wa Mataifa mnamo Septemba 24."
Kuhusiana na suala hilo, Qutaiba Adelbi, Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria, alikakanusha kabisa kufanyika mkutano wowote kati ya Ahmed al-Shara na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni mwezi ujao. Wakati huo huo, shirika la habari la Syria (SANA) liliripoti siku ya Jumanne kufanyika kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya mpito ya nchi hii na ujumbe wa utawala wa Kizayuni mjini Paris.