Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel akiri kutengwa utawala huo kisiasa
Aug 27, 2025 12:42 UTC
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kutengwa na kuzingirwa kisiasa utawala huo katika ngazi za kimataifa.
Katika mahojiano na gazeti la "Wall Street Journal" la Marekani lililochapishwa siku ya Jumatano, Gideon Sa'ar, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa utawala wa Kizayuni amezungumzia juhudi za kimataifa za kulitambua taifa la Palestina na kusema: 'Israel hivi sasa inakabiliwa na changamoto za kisiasa na kutengwa katika ngazi ya kimataifa, zaidi ya changamoto za kijeshi.'