Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran: Hatuna budi ila kuwa na nguvu
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i130076-kamanda_mkuu_wa_jeshi_la_jamhuri_ya_kiislamu_ya_iran_hatuna_budi_ila_kuwa_na_nguvu
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Iran haina chaguo jingine isipokuwa kujiimarisha kijeshi na kuwa na nguvu.
(last modified 2025-08-27T12:53:07+00:00 )
Aug 27, 2025 12:51 UTC
  • Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran: Hatuna budi ila kuwa na nguvu

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Iran haina chaguo jingine isipokuwa kujiimarisha kijeshi na kuwa na nguvu.

Amesema: "Tunahitaji jeshi lenye nguvu kwa ajili ya kulinda taifa letu, na jeshi lenye nguvu ni jeshi linalotekeleza vipengele vyake vyote, ujumbe na wajibu wake kwa usahihi."

Meja Jenerali Amir Hatami, amesema hayo siku ya Jumatano, katika hafla iliyofanyika kwa mnasaba wa Bu Ali Sina (Siku ya Madaktari) na Mohammad bin Zakariya Razi (Siku ya Wafamasia) katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Aja mjini Tehran. Akieleza kuwa jeshi linawajibika kwa dhamira kubwa ya kulinda kujitawala, umoja wa ardhi na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, Meja Jenerali Amir Hatami ameongeza kuwa: "Wajibu huu ni muhimu sana katika nchi yoyote ile, lakini una umuhimu maradufu na wa kipekee nchini Iran kutokana na nafasi yake ya kimkakati na kijiografia.