Yemen yashambulia uwanja wa ndege wa Ben-Gurion kwa kombora la masafa marefu
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i130108-yemen_yashambulia_uwanja_wa_ndege_wa_ben_gurion_kwa_kombora_la_masafa_marefu
Msemaji wa jeshi la Yemen ametangaza kuwa uwanja wa ndege wa Ben Gurion huko Tel Aviv umelengwa kwa shambulio la kombora la balestiki la nchi hiyo.
(last modified 2025-08-28T08:12:16+00:00 )
Aug 28, 2025 08:09 UTC
  • Yemen yashambulia uwanja wa ndege wa Ben-Gurion kwa kombora la masafa marefu

Msemaji wa jeshi la Yemen ametangaza kuwa uwanja wa ndege wa Ben Gurion huko Tel Aviv umelengwa kwa shambulio la kombora la balestiki la nchi hiyo.

Siku ya Jumatano, Yahya Sarei alitangaza operesheni maalum ya kijeshi ya kulenga Uwanja wa Ndege wa Ben-Gurion kwa kombora la masafa marefu la "Palestina 2" na kusema kuwa operesheni hiyo ilifanikiwa na kupelekea mamilioni ya Wazayuni kukimbilia kwenye mahandaki na kusimamisha operesheni za kawaida za uwanja huo wa ndege.

Akisisitiza kuwa operesheni hiyo ilifanywa kwa ajili ya kulisaidia taifa linalodhulumiwa la Palestina na Mujahidina wake na katika kukabiliana na jinai za mauaji ya halaiki na njaa zinazofanywa na adui wa wakazi wa Gaza, msemaji huyo wa jeshi la Yemen ameongeza kuwa, kutambuliwa duniani kote ukubwa wa mateso ya watu wa Gaza ikiwemo njaa, mzingiro na uchokozi, kunayawajibisha kihistoria mataifa ya Kiarabu na Kiislamu. Yahya Saree ametoa wito kwa Umma wa Kiarabu na Kiislamu, ambao una wajibu wa kidini, kiutu na kimaadili, kuchukua hatua za kukomesha njaa, kuondoa mzingiro na kusimamisha mashambulizi ya kichokozi ya Wazayuni dhidi ya watu wa Gaza.