Kolivand: Tunakaribia kwenye eneo la ajali ya helikopta ya Rais Ebrahim Raisi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i111958-kolivand_tunakaribia_kwenye_eneo_la_ajali_ya_helikopta_ya_rais_ebrahim_raisi
Mkuu wa Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa timu za uokoaji za shirika hilo zinakaribia eneo ilikotokea ajali ya helikopta iiliyokuwa imembeba Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wenzake katika mkoa wa Azarbaijan Mashariki, kaskazini magharibi mwa Iran.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
May 19, 2024 23:40 UTC
  • Kolivand: Tunakaribia kwenye eneo la ajali ya helikopta ya Rais Ebrahim Raisi

Mkuu wa Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa timu za uokoaji za shirika hilo zinakaribia eneo ilikotokea ajali ya helikopta iiliyokuwa imembeba Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wenzake katika mkoa wa Azarbaijan Mashariki, kaskazini magharibi mwa Iran.

Pir Hossein Kolivand amesema katika mahojiano ya televisheni ya taifa kwamba: timu za uokoaji zinakaribia kwenye helikopta iliyokuwa imembeba Rais Ebrahim Rais na wenzake na kwamba maelezo zaidi yatatolewa muda mfupi ujao. Amesema juhudi za uokoaji zinafanyika eneo la milimani la Tekavar huko Azarbaijan Mashariki.

Pir Hossein Kolivand

Jioni ya jana Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alieleza kusikitishwa na ajali ya helikopta iliyokuwa imembeba Rais wa Jamhuri ya Kiislamu na wenzake na kusema: Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amrudishe salama mheshimiwa Rais na wenzake.

Hali mbaya ya hewa na ukungu mkubwa unaifanya kazi ya uokoaji kuwa ngumu katika eneo la Jolfa huko kaskazini maghaibi mwa Iran.

mapema jana, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran alisema, msafara wa Rais Ebrahim Raisi ulikuwa angani katika helikopta kadhaa, na kwamba moja ya helikopta hizo ambayo ilimbeba Rais ililazimika kutua kwa kishindo kutokana na hali mbaya ya hewa.

Helikopta hiyo ilikuwa imembeba Raisi Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, Gavana wa mkoa wa Azarbaijan Mashariki Malek Rahmati, Imam wa Swala ya Ijumaa na mwakilishi wa Kiongozi wa Mapiinduzi ya Kiislamu huko Tabriz, Mohammad Ali Al- Hashem na maafisa wengine kadhaa wa serikali.