Araqchi: Makombora ya Yemen yamevuruga mahesabu ya Marekani na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i120572-araqchi_makombora_ya_yemen_yamevuruga_mahesabu_ya_marekani_na_israel
Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa usahihi wa makombora ya Yemen umevuruga kwa kiasi kikubwa mahesabu ya kimkakati ya muungano wa Israel na Marekani.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Dec 25, 2024 00:18 UTC
  • Araqchi: Makombora ya Yemen yamevuruga mahesabu ya Marekani na Israel

Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa usahihi wa makombora ya Yemen umevuruga kwa kiasi kikubwa mahesabu ya kimkakati ya muungano wa Israel na Marekani.

Sayyid Abbas Araqchi amepongeza oparesheni zilizozaa matunda za Yemen za kuwaungwa mkono wananchi wa Palestina. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza haya jana katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran wakati alipokuwa akibainisha hatua kubwa athirifu zilizotekelewa na nchi ya Kiarabu ya Yemen katika kuwaunga mkono watu wa Gaza na kambi nyingine za muqawama. 

Abbas Araqchi ameashiria pia mashambulizi ya siku kadhaa zilizopita ya jeshi la Yemen ambapo lilitumia kombora lake la hypersonic na kupiga ndani kabisa ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).

" Wananchi wa Yemen  kwa kutegemea makombora waliyoyaunda wenyewe na zana za kujihami, wamecheza nafasi isiyo na kifani na kushiriki pakubwa katika kuwahami wananchi wa Palestina tangu kuanza Oparesheni ya  Al-Aqsa dhidi ya adui Mzayuni", amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran.

Katika sehemu nyingine ya mkutano wake na waandishi wa habari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kwa mara nyingine tena juu ya uungaji mkono usiolegalega wa Tehran kwa wanachama wote wa mhimili wa muqawama.