Jeshi la Iran, IRGC kufanya mazoezi ya kijeshi yenye 'nguvu'
Kamanda wa ngazi ya juu wa Iran ametangaza kwamba vikosi vya jeshi la Iran vitaandaa mazoezi tata ya kijeshi yenye na ambayo yatajumuisha Jeshi la Kitaifa (Artesh) na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
Meja Jenerali Gholam-Ali Rashid, Kamanda wa Makao Makuu ya Kamandi ya Khatam al-Anbiya, alitoa tangazo hilo siku ya Jumatano, wakati wa kikao na wakuu wa kijeshi kutoka Vikosi vya Wanajeshi wa Iran.
Alisema: "Vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu vitafanya mazoezi yenye nguvu ya kuhujumi na kujihami katika siku na wiki zijazo."
Kulingana na Jenerali Rashid, Jeshi na IRGC hushiriki mara kwa mara katika mazoezi ya pamoja, haswa katika nusu ya pili ya mwaka wa kalenda ya Kiirani katika maeneo mbalimbali ya nchi kavu, anga na baharini.
Maneva hayo, kamanda huyo alibainisha, yatajumuisha vifaa vya kijeshi vya kujihami na vya kuhujumu, na yanafanyika kwa lengo la kujitayarisha "kukabiliana na maadui wa taifa la Iran."
Afisa huyo amesema kila mwaka, takriban mazoezi 30 wa kijeshi hufanyika nchini Iran.
Amebainisha kuwa kwa kuwa mazoezi hayo yatawezesha Majeshi ya Iran kuwa tayari kukabiliana na vitisho, na kuhakikisha kuwa nchi iko tayari kujihami na kumuangamiza adui.
Jenerali Rashid alisema utawala wa Israel umejidanganya na umefanya makosa ya kimahesabukuhusiana na Jamhuri ya Kiislamu. Aidha amesema operesheni kali za mashambulio yaliyotekelezwa hivi karibuni na Iran dhidi ya dhidi ya utawala huo ghasibu hususan Operesheni yake ya Ahadi ya Kweli II, "zimeonyeshwa sehemu ndogo tu ya uwezo wa kijeshi wa Iran.
Kamanda huyo amesisitiza kwamba kwa kuzingatia itikadi ya kujihami ya Jamhuri ya Kiislamu, Iran kamwe si mwanzilishi wa vita vyovyote katika eneo.
Jenerali Rashid alisisitiza kwa hiyo, mazoezi yajayo yenye nguvu yatafanyika sambamba na kuhakikisha nchi iko tayari kujihami na kushambulia kukabiliana na tishio la aina yoyote.