Rais Pezeshkian: Tunatazamia uhusiano wa kirafiki na nchi za kanda na ulimwengu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i120652-rais_pezeshkian_tunatazamia_uhusiano_wa_kirafiki_na_nchi_za_kanda_na_ulimwengu
Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesisitiza kuwa, Iran inatazamia kwa hamu kuwa na uhusiano wa kirafiki na nchi za eneo na dunia na inafanya hima kuhakikisha kunakuweko amani na usalama ndani na nje.
(last modified 2024-12-26T23:29:04+00:00 )
Dec 26, 2024 23:29 UTC
  • Rais Pezeshkian: Tunatazamia uhusiano wa kirafiki na nchi za kanda na ulimwengu

Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesisitiza kuwa, Iran inatazamia kwa hamu kuwa na uhusiano wa kirafiki na nchi za eneo na dunia na inafanya hima kuhakikisha kunakuweko amani na usalama ndani na nje.

Rais Pazshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye anazuru Mkoa wa Khorasan Kaskazini (kaskazini mashariki), amesema hayo katika hotuba yake aliyoitoa mbele ya hadhara ya watu wa mkoa huo katika jiji la Bojnord na kusisitiza kwamba, hatupaswi kuvutana na ulimwengu na wala hatuna nia ya kushambulia ardhi ya wengine, kama ambavyo hatutamruhusu mtu yeyote kushambulia mipaka yetu au haki zetu.

Daktari Pezeshkiana amebainisha kwamba, kulinda  na kuhifadhi umoja wa ardhi ya  nchi yetu ni kanuni yetu, lakini wakati huo huo maono yetu yamejikita juu ya amani na usalama kama ambavyo tuna uwezo wa kutatua matatizo yetu ya ndani kwa upendo na maelewano.

Rais Pezeshkian pia amesisitiza umoja baina ya nchi za Kiislamu na kusema: "Kwa bahati mbaya, tunashuhudia mizozo na ahitilafu nyingi kati ya nchi za Kiislamu na kuongeza kuwa, ikiwa Waislamu katika eneo watashikamana na umoja na kuudumisha hakuna nguvu itakayoweza kukanyaga na kupora haki zao.