Iran yaongeza uuzaji mafuta ghafi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i121002-iran_yaongeza_uuzaji_mafuta_ghafi
Mauzo ya nje ya mafuta ghafi kutoka Iran yalipanda tena katika nusu ya pili ya Desemba, baada ya kuanza polepole katikati ya mwezi huo.
(last modified 2025-01-04T09:09:57+00:00 )
Jan 04, 2025 09:09 UTC
  • Iran yaongeza uuzaji mafuta ghafi

Mauzo ya nje ya mafuta ghafi kutoka Iran yalipanda tena katika nusu ya pili ya Desemba, baada ya kuanza polepole katikati ya mwezi huo.

TankerTrackers, kampuni ya uchambuzi wa usafirishaji mafuta ghafi baharini, iliripoti ongezeko la mauzo ya nje ya mafuta ghafi ya Iran katika nusu ya pili ya Desemba 2024, baada ya ukuaji wa polepole mapema mwezi huo.

Kulingana na ripoti yana data kutoka TankerTrackers, mauzo ya nje ya mafuta ya Iran yaliongezeka mwishoni mwa Desemba.

Ingawa kampuni haikutoa takwimu maalum, ilionyesha ongezeko kubwa baada ya mauzi ya chini nusu ya kwanza ya mwezi huo.. TankerTrackers pia ilibainisha kuwa Iran imesitisha kusafirisha mafuta kwenda Syria.

Ripoti hiyo imebaini kuwa haya yanatokana na robo ya mwaka yenye changamoto kwa sekta ya mafuta ya Iran. Licha ya kufikia viwango vya juu zaidi vya mauzo ya nje katika miaka sita mnamo 2024, ukuaji ulizuiwa mnamo Oktoba na Novemba kutokana na bei za juu za mafuta ghafi ya Iran yaliyouzwa kwa China.

Mwezi Oktoba tofauti ya bei kati ya mafuta ghafi ya Iran na Brent ilikuwa ndogo zaidi katika miaka mitano wakati wa mvutano wa kisiasa katika eneo la Asia ya Magharibi.

Vyombo vya habari vya Iran viliripoti katikati ya Desemba kwamba mauzo ya nje ya mafuta kwenda China, mnunuzi mkubwa wa mafuta ya Iran, yalipungua kwa mapipa 524,000 kwa siku (bpd) mnamo Novemba ikilinganishwa na Oktoba, kufikia mapipa milioni 1.31 kwa siku - kiwango cha chini kabisa katika miezi minne.

Licha ya vikwazo vya Marekani kwenye sekta ya mafuta yake, Iran imekuwa ikisafirisha zaidi ya mapipa milioni 1.0 kwa siku, hasa kwenda China. Waziri wa mafuta wa Iran amesema kuwa Iran inajiandaa kwa vikwazo vipya chini ya utawala mpya wa Marekani.

Uimara huu unaonyesha uwezo wa Iran wa kukabiliana na vikwazo pamoja na mashinikizo ya kiuchumi huku ikidumisha uwepo mkubwa katika soko la kimataifa la mafuta.