Pezeshkian: Iran inaunga mkono amani na kuondolewa mivutano katika eneo na duniani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i121454-pezeshkian_iran_inaunga_mkono_amani_na_kuondolewa_mivutano_katika_eneo_na_duniani
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mahojiano na televisheni ya NBC ya Marekani kwamba Iran inataka amani na kuondolewa mivutano katika kanda hii na duniani kwa ujumla.
(last modified 2025-01-15T04:29:48+00:00 )
Jan 15, 2025 04:29 UTC
  • Pezeshkian: Iran inaunga mkono amani na kuondolewa mivutano katika eneo na duniani

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mahojiano na televisheni ya NBC ya Marekani kwamba Iran inataka amani na kuondolewa mivutano katika kanda hii na duniani kwa ujumla.

Rais Masoud Pezeshkian jana usiku alifanyiwa mahojiano na televisheni ya NBC ya Marekani ambapo mbali na mashambulizi na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza alisisitiza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inataka amani na inataka amani na kuondolewa mivutano katika Asia Magharibi na duniani kote na ipo tayari kufanya mazungumzo ya mantiki, ya kuheshimiana na ya usawa baina ya pande mbili. 

Katika mahojiano hayo, ripota wa NBC alimuuliza Rais wa Iran swali la kushangaza kwa kusema: "moja ya mambo yanayoweza kuwa tishio kwa diplomasia ni kwamba Marekani inaamini kuwa Iran inapanga kumuua Donald Trump. Je kulikuwepo kweli na mpango kama huo?"

Katika kujibu swali hilo, Rais Pezeshkian alisema: "mashambulizi yote ya kigaidi tunayoyaona katika eneo, huko Ulaya, na kwingineko, imepatikana ndani yake athari yoyote ya Wairani?! Je kulikuwapo na uhusiano wowote, abadan! Kinachotajwa kama njama dhidi ya Trump ni mpango wa Israel na nchi nyingine wa kueneza uadui dhidi ya Iran". 

Rais Masoud Pezeshkian katika mahojiano na televisheni ya NBC