Araghchi asisitiza: Iran ina haki ya kumiliki mzunguko kamili wa fueli ya nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i125936-araghchi_asisitiza_iran_ina_haki_ya_kumiliki_mzunguko_kamili_wa_fueli_ya_nyuklia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi amesema, kurudia kila mara kauli za uwongo hakubadilishi ukweli wa kimsingi na akaeleza bayana kwamba, Iran, ikiwa ni miongoni mwa nchi zilizotia saini mkataba wa NPT, ina haki ya kumiliki mzunguko kamili wa fueli ya nyuklia.
(last modified 2025-12-29T03:39:49+00:00 )
May 03, 2025 06:57 UTC
  • Araghchi asisitiza: Iran ina haki ya kumiliki mzunguko kamili wa fueli ya nyuklia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi amesema, kurudia kila mara kauli za uwongo hakubadilishi ukweli wa kimsingi na akaeleza bayana kwamba, Iran, ikiwa ni miongoni mwa nchi zilizotia saini mkataba wa NPT, ina haki ya kumiliki mzunguko kamili wa fueli ya nyuklia.

Seyyed Abbas Araqchi ameeleza hayo katika ujumbe alioweka kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X na kubainisha: "mimi, kimsingi, naepuka kurusha hewani kupitia vyombo vya habari hoja zinazohusu vipengele muhimu vya mazungumzo ".
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongezea kwa kusema: "lakini ninachotaka kusema ni kwamba, kurudia uwongo hakubadilishi ukweli wa kimsingi." Iran, ikiwa ni mmoja wa watiaji saini waanzilishi wa mkataba wa NPT ina haki ya kumiliki mzunguko kamili wa fueli ya nyuklia. Isitoshe, mbali na Iran kuna wanachama kadhaa wa NPT ambao wanarutubisiha urani ilhali wanapinga pia kikamilifu silaha za nyuklia. Mbali na Iran, klabu hii inajumuisha pia nchi kadhaa za Asia, Ulaya na Amerika ya Kusini".
 
 Araghchi ameendelea kueleza kwamba, kutangaza msimamo wa vikwazo vya juu kabisa na kuporoja kauli za uchochezi hakutakuwa na matokeo mengine yoyote zaidi ya kuharibu fursa ya kupatikana mwafaka katika mazungumzo.
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametanabahisha kwa kusema, makubaliano yenye itibari na ya kudumu yanaweza kufikiwa, kitu pekee kinachohitajika ni nia thabiti ya kisiasa na mtazamo wa kiinsafu.../