Araqchi: Waandishi wa habari walisimama kidete wakati wa vita vya siku 12
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza kuwadia Siku ya "Waandishi wa habari" na amewakumbuka na kuwaenzi waandishi wa habari waliouliwa shahidi khususan katika vita vya kulazimishwa vya hivi karibuni.
Sayyid Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Jumatatu alihudhuria katika mkutano wa kila wiki wa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na waandishi wa habari hapa Tehran na akasema: Awali ya yote, anaheshimu suala la kuwakumbuka na kuwaenzi mashahidi wote hasa waandishi wa habari waliouawa shahidi wakitekeleza majukumu yao, na bila shaka mashahidi wa vita vya siku 12
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa: Vita hivi vitakuwa moja ya nukta za kukumbukwa katika historia ya Iran. Vita ambavyo ndani yake madola makubwa na utawala dhalimu wa Kizayuni huku yakiungwa mkono na kushirikiana na pande nyingine nyingi yalitekeleza uvamizi wa kijeshi wakitumai kuwa wangeweza kufanikisha malengo yao kupitia hujuma ya kushtukiza lakini wananchi wa Iran walidhihirisha kuwa hawawezi kusambaratishwa kwa njia hizo.
Amesema, wananchi wa Iran walionyesha umoja na mshikamano na kusimama imara dhidi ya adui. Katika hili, waandishi wa habari walikuwa na mchango na nafasi maalumu.
Araqchi ameendelea kubainisha kuwa: Waandishi wa habari walikuwa bega kwa bega katika siku zote za vita vya Israel dhidi ya Iran.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongezea kwa kusema: Siku ya Waandishi wa Habari imetajwa kuwa ni siku ya kumkumbuka Shahidi Saremi; na jambo muhimu ni kwamba: Shahidi Saremi aliuliwa shahidi pamoja na wanadiplomasia kadhaa.
Wanadiplomasia na waandishi wa habari kadhaa waliuawa shahidi wakiwa pamoja huko Mazar-e-Sharif, na nukta muhimu ni kuwa pamoja wanadiplomasia na waandishi wa habari.