Shamkhani: Siasa za ugaidi mamboleo za Marekani zimelenga utambulisho wa nchi mbalimbali
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i54202-shamkhani_siasa_za_ugaidi_mamboleo_za_marekani_zimelenga_utambulisho_wa_nchi_mbalimbali
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa siasa za ugaidi mamboleo za Marekani ambazo zinajumuisha masuala kama nyenzo za intelijinsia, vita vya kisaikojia, hujuma za kimtandao, vita vya kielektroniki, na kuhatarishwa mazingira zinalenga utambulisho na mamlaka ya kitaifa ya nchi mbalimbali duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 18, 2019 08:51 UTC
  • Shamkhani: Siasa za ugaidi mamboleo za Marekani zimelenga utambulisho wa nchi mbalimbali

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa siasa za ugaidi mamboleo za Marekani ambazo zinajumuisha masuala kama nyenzo za intelijinsia, vita vya kisaikojia, hujuma za kimtandao, vita vya kielektroniki, na kuhatarishwa mazingira zinalenga utambulisho na mamlaka ya kitaifa ya nchi mbalimbali duniani.

Ali Shamkhani ameashiria hatua za Marekani na utawala wa Kizayuni za kutumia virusi vya stuxnet kwa lengo la kudhuru taasisi za nyuklia za Iran na kueleza kuwa: Kukaa kimya au kutolewa radiamali dhaifu kimataifa kwa hujuma hiyo ya kimtandao kumepelekea hii leo Marekani kuwa na ujasiri wa kushambulia pia taasisi za umeme za Venezuela. 

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameitaja Marekani ya hivi sasa ya utawala wa Trump kuwa nchi inayopenda vita zaidi katika historia nzima ya nchi hiyo. Amesema Marekani inatumia mifumo ya fedha, kibenki na kanali za fedha za kimataifa kama silaha za kuzishambulia nchi nyingine zilizo huru. Ali Shamkhani ameashiria pia kukiukwa kwa makusudi sheria za kimataifa na kujitoa Marekani katika makubaliano mbalimbali ya kimataifa na kueleza kuwa nchi huru duniani zinapasa kusimama kidete kwa kuasisi mfumo wa kiutendaji wa pande kadhaa ili kukabiliana na nchi hiyo. Ameongeza kuwa moja ya njia za kukabiliana na vitisho hivi vya Marekani ni kufanya juhudi za pamoja ili kunusuru uchumi wa dunia na kutokuwa chini ya uhodhi wa sarafu ya dola, kuwepo na mfumo wa fedha wa kimataifa nje ya udhibiti wa Marekani, kuendesha mapambano dhidi ya vikwazo vya serikali ya Marekani dhidi ya nchi nyinginezo na kushirikiana kwa pamoja nchi mbalimbali kwa shabaha ya kukabiliana na vitisho vipya vya kiusalama. 

Marekani inatumia sarafu ya dola kama wenzo wa kuhodhi uchumi wa dunia