-
Iran yakanusha tuhuma chapwa za Marekani, Uingereza na Ufaransa
Jul 24, 2024 02:58Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amemwandikia barua Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Matiafa na kukanusha tuhuma za uongo zilizotolewa na Marekani, Uingereza na Ufaransa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza kuwa tuhuma hizo zinatokana na chuki za madola hayo kwa taifa la Iran ya Kiislamu.
-
Katika barua kwa kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, vijana wa Ubelgiji: Tumefurahishwa sana na ujumbe wako
Jul 24, 2024 00:05Katika barua yao kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, idadi kubwa ya vijana wa Ubelgiji wamemshukuru Ayatullah Ali Khamenei kwa barua yake ya hivi karibuni ya kuunga mkono maandamano ya kuonyesha mshikamano na watu wa Gaza katika vyuo vikuu vya Marekani na Ulaya na kutangaza kwamba, wameathiriwa sana na ujumbe na wito wake.
-
Iran iko tayari kushirikiana katika mapambano dhidi ya magendo ya madawa ya kulevya
Jul 23, 2024 23:07Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema katika kikao cha Mkutano wa Pili wa Kikanda wa Kupambana na Madawa ya Kulevya huko Baghdad kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kikamilifu kushirikiana na taasisi na mifumo ya kikanda na kimataifa kuendesha vita dhidi ya mihadarati.
-
Iran yavunja ukiritimba katika bidhaa za nyuklia
Jul 23, 2024 10:16Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema Iran imeweza kuvunja ukiritimba katika sekta ya nyuklia huku bidhaa na huduma zake zilizoundwa nchini hivi leo zikiuzwa katika soko la kimataifa.
-
Iran: Kusimama imara watu wa Yemen ni fakhari kwa Umma wa Kiislamu
Jul 23, 2024 03:50Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kusimama imara uongozi, wapiganaji wanajihadi na wananchi wanamuqawama wa Yemen na kuwa bega kwa bega na watu madhulumu wa Palestina katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni ni hatua ya kihistoria na ya kujivunia kwa Umma wa Kiislamu.
-
IRGC yanasa meli ya 'Togo' ikifanya magendo ya mafuta Ghuba ya Uajemi
Jul 22, 2024 23:27Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limefanikiwa kutwaa meli nyingine ya kigeni ikifanya magendo ya mafuta mengi katika maji ya Ghuba ya Uajemi.
-
Kan'ani: Kubadilika kwa watu na serikali huko Marekani si muhimu kwa Iran
Jul 22, 2024 22:56Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema mabadiliko ya serikali huko Marekani si muhimu na hayana taathira yoyote katika sera za kigeni za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kiongozi Muadhamu asisitiza juu ya ushirikiano wa bunge na rais kwa ajili ya kuunda serikali inayofaa kiutendaji
Jul 22, 2024 08:19Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameelezea matumaini yake kuwa kupitia ushirikiano wa Rais Mteule na Bunge, baraza la mawaziri lenye watu waaminifu na wachapakazi litaundwa kwa ajili ya kutatua matatizo ya nchi na wananchi.
-
Pezeshkian: Wanaoiwekea vikwazo Iran waliwapa maadui silaha za kemikali
Jul 22, 2024 07:58Rais mteule wa Iran ameyakosoa vikali madola ambayo yameiwekea vikwazo Jamhuri ya Kiislamu akisisitiza kuwa, mataifa hayo yana historia nyeusi kwa kupeana silaha zilizotumiwa dhidi ya taifa hili katika miaka ya 1980.
-
Iran na Sudan zarejesha uhusiano; balozi wa Iran Khartoum akabidhi hati za utambulisho
Jul 21, 2024 23:44Kiongozi wa Baraza la Utawala wa Mpito na Mkuu wa Majeshi ya Sudan, Abdul Fattah Al-Burhan, amepokea hati za utambulisho za balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Sudan, Hassan Shah Hosseini.