-
Algeria: Ufaransa inakataa kutoa ramani ya maeneo yaliyotumiwa kwa majaribio ya nyuklia
Jul 05, 2021 05:49Waziri wa Mujahideen (maveterani wa vita vya ukombozi) nchini Algeria, Tayeb Zitouni amesema kuwa Ufaransa inakataa kuikabidhi nchi hiyo ramani ya maeneno yaliyotumiwa kwa ajili ya majaribio ya milipuko ya nyuklia yaliyofanywa na serikali ya Paris katika majangwa ya Algeria kwenye miaka ya sitini ya karne iliyopita.
-
Maandamano ya wiki hii ya wananchi wa Algeria yalikuwa ni ya Ijumaa ya 124
Jul 03, 2021 22:07Wananchi wa Algeria wanaendelea na maandamano yao ya kila wiki ambapo maandamano yaliyofanyika Ijumaa wiki hii, yalikuwa ya 124 ya kutaka mabadiliko ya kimsingi ya mfumo wa kisiasa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Jumuiya 82 za kutetea haki za binadamu zaitaka UN kusitisha ukandamizaji nchini Algeria
Jun 27, 2021 22:40Jumuiya 82 za kutetea haki za binadamu zimetoa wito wa kukomeshwa ukandamizaji unaofanywa na vyombo vya dola nchini Algeria.
-
Algeria yaifungia kanali ya Ufaransa ya "France 24"
Jun 14, 2021 03:41Serikali ya Algeria imeipokonya kanali ya televisheni ya Ufaransa ya France 24 leseni ya kuhudumu nchini humo, siku moja baada ya kufanyika uchaguzi wa Bunge katika nchi hiyo ya Kiarabu ya kaskazini mwa Afrika.
-
Algeria yapinga tena kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni
Jun 03, 2021 03:41Rais wa Algeria jana usiku kwa mara nyingine amesisitiza kuwa, nchi yake abadan haitaanzisha uhusiano na utawala ghasibu wa Israel.
-
Algeria yalitaka Baraza la Usalama la UN kuwahami Wapalestina katika Msikiti wa al Aqsa
May 10, 2021 08:05Wizara ya Mambo Nchi za Nje ya Algeria imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liwahami na kuwalinda Wapalestina wanaofanya itikafu ndani ya Msikiti wa al Aqsa.
-
'Maulamaa wa Algeria waendeshe Jihadi ili kutokomeza mabaki ya utamaduni wa Kifaransa'
May 06, 2021 21:54Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Algeria lillo chini ya ofisi ya rais wa nchi hiyo amesema, Maulamaa wa Kiislamu wa nchi hiyo inapasa waendeleze jihadi ya kielimu na kitaifa kwa ajili ya kung'oa na kutokomeza mabaki ya utamaduni wa Kifaransa.
-
Usalama wa kikanda; ajenda ya mazungumzo ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Algeria na Libya
Apr 20, 2021 03:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria jana Jumatatu alikutana na mwenzake wa Libya na kufanya mazungumzo kuhusu usalama wa kikanda na kuziunga mkono pande za Libya kwa lengo la kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.
-
Mshauri wa Rais wa Algeria: Ufaransa ilieneza ujinga nchini zama za ukoloni
Apr 19, 2021 06:51Mshauri wa Rais wa Algeria amesema kuwa Ufaransa ilifanya kazi ya kueneza ujinga wa kutojua kusoma na kuandika wakati wa ukoloni wa nchi hiyo nchini Algeria.
-
Maelfu waandamana dhidi ya serikali nchini Algeria
Apr 17, 2021 01:33Maelfu ya watu wamefanya maandamano katika miji mbalimbali ya Algeria wakitaka kuachiwa huru wanaharakati wa kisiasa na kutoa wito wa kususiwa uchaguzi mkuu wa mapema wa Bunge nchini humo.