-
Iran yatangaza mashtaka rasmi dhidi ya Marekani na Israel kuhusu mauaji ya kigaidi ya Kiongozi Muadhamu na wanafunzi wa Minab
Aug 30, 2026 03:48Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa hati rasmi za mashtaka kufuatia vitendo vya kigaidi vilivyofanywa na muungano wa Marekani na Israel, ambavyo vilisababisha kuuawa kishahidi kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na wanafamilia wake wanne, sambamba na wanafunzi na walimu katika shule moja mjini Minab.
-
Iran yaendelea kuboresha sekta yake ya ulinzi baada ya vita vya Marekani na Israel
Aug 22, 2026 02:55Wizara ya Ulinzi ya Iran imesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu inaendelea kuifanya sekta yake ya ulinzi kuwa ya kisasa, ikizingatia mahitaji yaliyojitokeza kutokana na vita vya hivi karibuni vilivyolazimishwa dhidi ya nchi hii na Marekani na Israel.
-
Marasimu ya Arubaini ya kumuenzi Kiongozi shahidi wa Iran na familia yake yafanyika Musalla wa Imam Khomeini, Tehran
Aug 18, 2026 15:39Sambamba na kutimia siku arubaini tangu kufanyika mazishi ya kihistoria ya kiongozi wa Iran aliyeuliwa shahidi, shughuli ya kumbukumbu ya kumuenzi kiongozi huyo shahidi na familia yake imefanyika leo katika eneo la Swala (Mosalla) la Imam Khomeini (RA) mjini Tehran.
-
Ayatullah Mojtaba Khamenei asifu ushiriki ‘wa kihistoria’ wa waumini katika mazishi, aapa kulipiza kisasi kwa Kiongozi Shahidi
Jul 11, 2026 12:01Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ametoa shukrani zake za dhati kwa mahudhurio “ya kustaajabisha, yenye kuvunja nguvu za adui na ya kihistoria” katika mazishi ya Kiongozi Shahidi, akisisitiza kuwa malipo ya kisasi dhidi ya “watenda jinai wauaji waliodhalilika” ni jambo la yakini.
-
Kiongozi Shahidi Ayatullah Khamenei azikwa katika Haram ya Imam Ridha (a.s) mjini Mash'had
Jul 11, 2026 02:37Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Sayyid Aali Khamenei amezikwa katika Haram ya Imam Ridha (a.s) mjini Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran.
-
Rais Pezeshkian: Mazishi ya Kiongozi wa Iran ni kielelezo cha umoja wa kitaifa
Jul 09, 2026 03:33Rais Masoud Pezeshkian amesema mahudhurio makubwa ya watu kutoka matabaka yote ya jamii katika mazishi makubwa yaliyofanyika kwa ajili ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ni kielelezo cha umoja wa kitaifa nchini Iran.
-
Mamilioni wamuaga Kiongozi Shahidi Ayatullah Khamenei katika miji ya Najaf na Karbala nchini Iraq
Jul 08, 2026 14:19Mamilioni ya waombolezaji leo Jumatano walikusanyika katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala nchini Iraq kwa ajili ya kuaga na kutoa heshima zao za mwisho kwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei na familia yake waliouliwa shahidi katika mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
-
Pezeshkian: Kufa shahidi Ayatullah Khamenei kumetoa msukumo kwa Waislamu kudumisha umoja
Jul 05, 2026 11:15Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu hayati Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, na kuuawa kwake shahidi, vimewapa Waislamu kote duniani hamasa katika harakati zao za kudumisha umoja na mshikamano.
-
Makundi ya Ulaya yanayopinga ubeberu yawasili Iran kwa mazishi ya Kiongozi Shahidi
Jul 03, 2026 03:53Misafara ya wanaharakati wanaopinga ubeberu, wasomi, waandishi wa habari na wawakilishi wa vituo vya Kiislamu kutoka kote barani Ulaya inaendelea kuwasili Tehran kushiriki katika mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei aliyeuawa shahidi katika shambulizi la kushtukiza la Marekani na Israel.
-
Pezeshkian: Mahudhurio makubwa katika mazishi ya Kiongozi Shahidi ni ‘jibu madhubuti’ kwa ubeberu na ugaidi
Jul 03, 2026 03:51Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesisitiza kuwa umati mkubwa wa wananchi utakaojitokeza katika shughuli ya mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, utakuwa “jibu madhubuti” dhidi ya vitendo vya kigaidi, ukatili na mbinu za kibeberu. Amesema kuwa tukio hilo litakuwa dhihirisho la wazi la umoja wa taifa la Iran na dhamira yake isiyotetereka katika kulinda uhuru na heshima ya nchi.