Pezeshkian: Kufa shahidi Ayatullah Khamenei kumetoa msukumo kwa Waislamu kudumisha umoja
-
Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu hayati Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, na kuuawa kwake shahidi, vimewapa Waislamu kote duniani hamasa katika harakati zao za kudumisha umoja na mshikamano.
Pezeshkian alibainisha haya jana katika hotuba yake katika "Mkutano wa Kimataifa wa Imam Khamenei- Kiongozi wa Milele wa Muqawama".
Amesema, Ayatullah Khamenei alikuwa akisisitiza mara kwa mara kuhusu umoja baina ya Waislamu kama hitaji muhimu kwa Umma wa Kiislamu, huku akitumia sehemu kubwa ya maisha yake kufafanua suala hilo kupitia hotuba, makala, na vitabu.
Rais wa Iran ameongeza kuwa kufa shahidi Kiongozi huyo Kiongozi wa Mapinduzi mnamo tarehe 28 Februari yaani siku ya kwanza ya mahambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran pia kuliwahamasisha mamilioni ya Waislamu kote duniani katika harakati zao za kudumisha umoja kati yao.
"Fikra na ujumbe wa viongozi wa kidini haviishii kwenye kuuawa kwao shahidi; bali vinabaki hai na kuongoza vizazi vijavyo kuendeleza njia ya ukweli, haki, na mapambano," amesema Pezeshkian katika Mkutano wa Kimataifa wa Imam Khamenei-Kiongozi wa Milele wa Muqawama.
Rais Pezeshkian aliendelea kubainisha kuwa: Imekuwa sera ya maadui wa Ulimwengu wa Kiislamu kuwalenga na kuwaua wanasayansi, wasomi, na watu wenye ushawishi ili kudhoofisha mataifa ya Kiislamu.
Katika hotuba yake hiyo, Rais wa Iran pia amekosoa kimya cha jamii ya kimataifa mkabala wa jinai kama hizo na kusema: "Leo hii tunashuhudia utawala wa Israel ukizungumzia waziwazi mauaji na kuwangamiza shakhsia mbalimbali. Ingawa mashirika ya kimataifa na watetezi wa haki za binadamu walipasa kuzuia vitendo kama hivyo, lakini kivitendo utawala huo unapewa himaya na kuungwa mkono kisiasa na kiutendaji.