-
Mahakama ya Iraq yaamuru Trump akamatwe kwa mauaji ya makamanda wa muqawama
Jan 08, 2021 02:44Mahakama ya Ar-Rasaafah nchini Iraq inayofuatilia kesi ya mauaji ya makamanda wa muqawama Luteni Jenerali Qassem Suleimani na Abu Mahdi al-Muhandis imetoa waranti wa kukamatwa rais wa Marekani Donald Trump.
-
Makombora yenye shabaha kali ya Lebanon, Syria, Yemen na Iran ndilo tishio kubwa zaidi kwa Israel 2021
Jan 08, 2021 02:43Kituo cha tafiti za usalama wa ndani cha utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kimetangaza kuwa tishio kubwa zaidi kwa utawala huo katika mwaka huu wa 2021 ni makombora yenye shabaha kali ya Lebanon, Syria, Yemen na Iran.
-
Hatimaye Trump asalimu amri, aahidi mapokezano ya madaraka yatafanyika kulingana na utaratibu
Jan 07, 2021 17:09Baada ya Kongresi ya Marekani kuthibitisha ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa rais, hatimaye rais wa nchi hiyo Donald Trump ametangaza kuwa mchakato wa kukabidhi madaraka kwa rais mteule utafanyika kama ulivyo utaratibu rasmi.
-
Rouhani: Demokrasia ya nchi za Magharibi ni dhaifu na isiyo na misingi
Jan 07, 2021 11:56Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema matukio ya hivi karibuni nchini Marekani ikiwa ni pamoja na kuvamiwa jengo la Bunge la Congress yanaashiria udhaifu na kutokuwa na msingi demokrasia ya nchi za Magharibi.
-
Marekani katika lindi la machafuko ya kisiasa
Jan 07, 2021 09:56Machafuko, fujo, vurugu, uporaji, ufyatuaji risasi, mauaji, ugaidi, mapinduzi, kukabiliana na mapinduzi; bali kwa kifupi; kashfa ya taifa, ndiyo maneno ambayo kila moja linafasiri matukio ya aibu yaliyotokea jana Jumatano, Januari 6, 2021 nchini Marekani ndani jengo la Congress
-
UN: Wanasiasa Marekani waheshimu mchakato wa kidemokrasia na utawala wa sheria
Jan 07, 2021 09:43Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na yaliyojiri Jumatano mjini Washington DC nchini Marekani na kuwataka viongozi wa kisiasa kuwaasa wafuasi wao kujizuia na ghasia.
-
Trump adai kuchakachuliwa kura katika uchaguzi mdogo wa Georgia
Jan 06, 2021 12:25Rais wa Marekani amekituhumu chama cha Democratic kuwa kimefanya udanganyifu katika uchaguzi mdogo wa Baraza la Sanate la nchi hiyo.
-
Trump: White House na Seneti hazitaingia kwenye mikono ya Wademocrat
Jan 05, 2021 07:12Kwa mara nyingine tena Rais Donald Trump wa Marekani amekataa kuyakubali matokeo ya uchaguzi wa rais wa nchi hiyo uliofanyika Novemba 3 mwaka uliopita, ambayo yanaonyesha kuwa ameshindwa.
-
Kukosoa ripota wa Umoja wa Mataifa hatua isiyo ya kisheria ya Marekani ya kumuua Qassim Suleimani
Jan 04, 2021 11:03Januari 3 mwaka uliomalizika hivi majuzi wa 2020, kwa amri ya Rais Donald Trump, utawala wa kigaidi wa Marekani ulifanya jinai ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassim Suleimani, Mkuu wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Mkuu wa Harakati ya al Hashd al-Shaabi katika shambulio la anga lililofanywa jirani na uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq.
-
Trump amtaka makamu wake asiidhinishe matokeo ya kura za Electoral College
Dec 26, 2020 02:41Rais Donald Trump wa Marekani amemtaka makamu wake Mike Pence asiidhinishe matokeo ya kura za urais zilizopigwa na wawakilishi wateule wa majimbo ya nchi hiyo, Electoral College.