-
Vipi Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limefikia natija ya kufanyika mauaji ya kimbari huko Gaza?
Sep 29, 2025 02:16Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limetangaza hatua za Israel huko Gaza kuwa ni mfano wa kisheria wa "mauaji ya halaiki."
-
Baada ya kuangamizwa askari 6 wa kizayuni, HAMAS yaionya Israel: Ghaza itageuka 'kaburi' la askari wenu
Sep 19, 2025 11:08Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imeuonya utawala wa kizayuni wa Israel kwamba hatua yake ya kuzidi kujiingiza ndani ya Mji wa Ghaza kutaugeuza mji huo kuwa "kaburi," la wanajeshi wa kizayuni baada ya sita miongoni mwao kuangamizwa na wanamuqawama wa Palestina katika matukio tofauti wakati wa jeshi la Israel likiwa linaendeleza mashambulizi makali na ya kinyama yanayolenga kulikalia kwa mabavu eneo lote la Ghaza.
-
Papa asema, Wapalestina wanahamishwa 'kwa mara nyingine tena' katika ardhi yao, ataka vita vya Ghaza vikomeshwe
Sep 18, 2025 03:45Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV amesema Wapalestina wanaishi katika "mazingira yasiyokubalika" huku wakihamishwa kwa nguvu katika Mji wa Ghaza, wakati huu wa mashambulizi makubwa yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel.
-
Ghaza yaandamwa na mashambulio ya kiwendawazimu ya Wazayuni, wanakaribia kuikalia kikamilifu
Sep 16, 2025 07:03Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limeanzisha mashambulizi makali ya anga dhidi ya Mji wa Ghaza kwa saa kadhaa, ambapo mbali na kuwaua shahidi Wapalestina kadhaa linateketeza pia majengo na miundomsingi iliyosalia katika eneo hilo.
-
UNRWA: Sambamba na mauaji ya kimbari, Israel imeifanya Ghaza 'ardhi ya nyika' isiyofaa kuishi binadamu
Sep 15, 2025 06:24Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena umesema una wasi wasi mkubwa juu ya hali mbaya sana ya maisha katika Ukanda wa Ghaza sambamba na kushadidi mashambulizi ya mabomu na makombora yanayofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo lililowekewa mzingiro.
-
Madaktari 17 wa kigeni waliohudumu Ghaza: Tumepokea watoto 114 waliopigwa risasi kichwani na kifuani
Sep 14, 2025 11:02Madaktari wa kimataifa wanaohudumu katika Ukanda wa Ghaza wameripoti hali ya kushtusha na kuhuzunisha ya majeraha ya risasi walizopigwa watoto Wapalestina, na kuibua wasiwasi wa kwamba watoto hao wamelengwa kwa makusudi. Hayo ni kwa mujibu wa uchunguzi uliochapishwa na gazeti la kila siku la Uholanzi la de Volkskrant.
-
Maseneta wa US: Israel inaangamiza kizazi Ghaza na Marekani ni mshirika, dunia lazima ikomeshe
Sep 14, 2025 10:48Maseneta wawili waandamizi wa Marekani wameishutumu Israel kwa kutekeleza kampeni ya maangamizi ya kizazi katika Ukanda wa Ghaza na kubainisha kwamba Marekani inashiriki katika jinai hiyo na kwamba dunia lazima ichukue hatua kukomesha jambo hilo.
-
Waziri Mkuu wa Uhispania: Nasikitika hatuna bomu la nyuklia tukaizuia Israel isishambulie Ghaza!
Sep 12, 2025 10:28Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez ameendelea kukosoa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina huku akieleza kwa masikitiko kwamba Uhispania haina bomu la nyuklia, manowari ya kubebea ndege za kivita, wala utajiri mkubwa wa mafuta, vitu vitakavyoiwezesha kusimamisha peke yake mashambulizi ya utawala huo dhidi ya Ghaza; lakini hiyo haimaanishi kwamba Madrid itasitisha juhudi zake.
-
HAMAS: Pendekezo la Marekani halilengi kumaliza vita vya Ghaza
Sep 09, 2025 11:04Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, Bassem Naim amesema, mapendekezo ya awali yaliyowasilishwa na Marekani lengo lake lilikuwa ni kutaka yakataliwe, na si kuweza kufikiwa makubaliano ya kumaliza vita, kuhakikisha vikosi vamizi vinaondoka kikamilifu huko Ghaza na kutekelezwa mabadilishano ya wafungwa.
-
Wasomi waliowasilisha lalamiko dhidi ya UK: 'Ghaza ni matokeo ya moja kwa moja ya Azimio la Balfour'
Sep 09, 2025 10:29Kundi moja la Wapalestina limewasilisha lalamiko la kisheria dhidi ya serikali ya Uingereza likidai kutolewa ungamo na fidia kwa jinai za kihistoria zilizofanywa na Uingereza huko Palestina kuanzia mwaka 1918 hadi 1948.