-
Kimbunga cha Bulbul chauwa watu 20 katika pwani za India na Bangladesh
Nov 11, 2019 04:31Watu 20 wameaga dunia na wengine zaidi ya milioni mbili wameachwa bila ya makazi kufuatia kimbunga kikali cha Bulbul kuyaathiri maeneo ya pwani ya India na Bangladesh huku kikiambatana na upepo mkali na mvua kubwa.
-
Mahakama ya India yabariki Wahindu wajenge hekalu lao eneo walipoubomoa msikiti wa kihistoria wa Babri
Nov 09, 2019 12:09Katika hukumu ya uonevu na upendeleo wa wazi iliyotolewa kwa manufaa ya Wahindu wenye misimamo ya chuki na kufurutu mpaka, Mahakama ya Juu Kabisa ya India imeamua kuwapatia Wahindu eneo walipoubomoa msikiti wa kihistoria wa Babri ili wajenge hekalu lao la Ram.
-
Pakistan yaitaka India ikomeshe ukandamizaji wa askari wake dhidi ya wakazi wa Kashmir
Nov 09, 2019 04:27Mkuu wa eneo la Kashmir lililo chini ya udhibiti wa Pakistan, ameitahadharisha serikali ya India kutokana na ukandamizaji wa askari wa nchi hiyo kuwalenga wakazi wa eneo la Kashmir lililo chini ya udhibiti wa New Delhi.
-
Taarifa ya pamoja ya Kansela wa Ujerumani na Waziri Mkuu wa India kuhusu makubaliano ya JCPOA
Nov 03, 2019 04:21Makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) ambayo yalikuwa natija ya juhudi za kidiplomasia na mazungumzo ya awamu kadhaa kati ya Iran na kundi la 5+1; hivi sasa yanakabiliwa na hatari kubwa kufuatia hatua ya Marekani ya kujitoa kwenye makubaliano hayo na kutotekeleza ahadi nchi za Ulaya; hatua iliyokabiliwa na radiamali kali ya Iran ambayo pia imeamua kupunguza hatua kwa hatua uwajibikaji wake ndani ya makubaliano hayo.
-
Pakistan yalaani hatua ya India ya kuligawa eneo la Kashmir katika sehemu mbili
Nov 01, 2019 08:20Serikali ya Pakistan imelaani hatua ya India ya kuligawa eneo la Jammu na Kashmir katika sehemu mbili.
-
India yazidisha hatua kali za usalama kabla ya kuhitimishwa kesi ya Msikiti wa Babri
Oct 15, 2019 00:35Serikali ya India imezidisha hatua kali za usalama katika mji wa Ayodhya, jimbo la Uttar Pradesh huko kaskazini mwa nchi hiyo kabla ya kutolewa uamuzi muhimu sana wa Mahaka Kuu ya nchi hiyo juu ya mzozo wa eneo la Msikiti wa Babri linalogombaniwa baina ya Waislamu na Wahindu.
-
Ahadi ya India ya kuondoa marufuku ya mawasiliano eneo la Kashmir
Oct 13, 2019 23:07Baada ya kupita zaidi ya miezi miwili ya kutekelezwa marufuku ya mawasiliano katika eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India, hatimaye serikali ya New Delhi imetangaza kufuta baadhi ya vizuizi vilivyowekwa katika uwanja huo.
-
Saudia yalazimika kununua mafuta kutoka India baada ya kushambuliwa na jeshi la Yemen
Oct 05, 2019 23:18Baada ya wanamapambano wa Yemen kushambulia na kuteketeza taasisi za mafuta za Saudi Arabia, sasa Shirika la Taifa la Mafuta la nchini hiyo ARAMCO limekumbwa na mgogoro mkubwa kiasi cha kulazimika kununua mafuta kutoka India ambayo nayo inanunua mafuta kutoka Iran.
-
Vitisho vya Marekani vya kuwawekea vikwazo waitifaki wake iwapo watanunua silaha za Russia
Oct 04, 2019 05:33Mwenendo wa Marekani wa kuchukua hatua za upande mmoja na nchi hiyo kupanua ubeberu wake katika kipindi cha Rais Donald Trump, umeshika kasi zaidi na sasa umechukua sura mpya.
-
Mvua na mafuriko yaua karibu watu 150 nchini India
Oct 01, 2019 04:38Watu 148 wamepoteza maisha baada ya kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazonyesha kwa siku tano sasa nchini India.