-
Iran yasajili mafanikio 15 ya nyuklia katika sekta ya tiba
Apr 09, 2024 04:14Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema kuwa nchi hii imesajili mafanikio mapya 15 katika uwanja wa matibabu na dawa aina za Radiopharmaceutical.
-
Iran kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki
Apr 08, 2024 22:50Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema kuwa, nchi yake itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki utakaofanyika mwezi ujao wa Mei.
-
Wapiganaji wa HAMAS waangamiza askari na maafisa 14 wa jeshi la Israel katika muda wa saa chache
Apr 07, 2024 03:34Wapiganaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS wamewaangamiza askari na maafisa 14 wa jeshi la Israel katika muda wa saa chache, baada ya kuwashambulia wanajeshi walioko kusini mwa Ukanda wa Ghaza unaohimili vita vya kinyama vya mauaji ya kimbari yanayoendelezwa na jeshi hilo la Kizayuni katika eneo hilo.
-
Kiwewe cha Wazayuni wakisubiri jibu la kijeshi la Iran kutokana na jinai zao
Apr 06, 2024 22:56Utawala wa Kizayuni umesema una wasiwasi na jibu liltakalotolewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufuatia jinai za karibuni iliyofanywa na utawala huo ya kuishambulia sehemu ya jengo la ubalozi dogo wa Iran huko Syria. Kwa kuhofia jibu la kijeshi la Iran, utawala wa Kizayuni umetoa amri ya kufungwa balozi zake katika maeneo mbalimbali duniani.
-
Aliyeongoza mashambulizi ya kigaidi kusini mashariki mwa Iran, atiwa mbaroni
Apr 06, 2024 07:05Msemaji wa Komandi Kuu ya Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza habari ya kutiwa mbaroni gaidi aliyeongoza mashambulizi ya kigaidi huko kusini mashariki mwa Iran. Gaidi huyo ametiwa mbaroni kwenye mji wa Karaj wa mkoa wa Alborz wa magharibi mwa Tehran.
-
Rais wa Iran: Walimwengu watajionea kuangamia kwa utawala wa Kizayuni
Apr 06, 2024 03:27Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu maalumu za kuwashukuru wananchi walio macho na wenye kujali thamani ya mambo wa Iran kwa ushiriki wao mkubwa katika matembezi ya Siku ya Quds Duniani na kusema: Walimwengu watajionea kuangamia kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Washiriki wa matembezi ya Siku ya Quds Iran: Jibu kali na la kujutisha umeandaliwa utawala wa Kizayuni
Apr 05, 2024 10:24Washiriki wa matembezi ya Siku ya Quds Duniani yaliyofanyika mjini Tehran wamesisitiza katika azimio walilotoa mwishoni mwa matembezi hayo juu ya kuwaunga mkono watu wanaodhulumiwa wa Ghaza na wakalaani jinai ya utawala bandia wa Kizayuni ya kushambulia balozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Syria.
-
Wananchi wa Iran waandamana katika Siku ya Kimataifa ya Quds
Apr 05, 2024 04:22Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds yamefanyika leo katika miji na maeneo mbalimbali nchini Iran.
-
Raisi: Tehran yaweka katika ajenda yake ya kazi ushirikiano na nchi zote za Kiislamu
Apr 05, 2024 04:22Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika dhifa ya (futari) Iftar na mabalozi wa nchi za Kiislamu wanaoishi Tehran kwamba suala la kushirikiana na nchi zote za Kiislamu lipo katika ajenda ya utendaji ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Wanajeshi wa Israel wazuiliwa kwenda livu ya nyumbani kwa tahadhari na hofu ya shambulio la Iran
Apr 04, 2024 22:53Jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel limesitisha livu ya nyumbani kwa wanajeshi wake kutokana na kuwepo hofu inayoongezeka ya utawala huo kuandamwa na shambulio la kulipiza kisasi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iran kufuatia shambulio la kigaidi ulilofanya wiki hii kwenye ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria.